The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
1 9 8 /
UFALME WA MUNGU
Ufalme Wako Uje! Usomaji kuhusu Ufalme wa Mungu (muendelezo)
Kwa hiyo, siri ya Ufalme ni utimilifu bila ukamilifu. Ufalme wa Mungu umekuja katika historia katika nafsi na huduma ya Yesu Kristo bila kukamilishwa. Siri hii ilikuwa imefichwa mpaka sasa ambapo imefunuliwa katika Kristo. 13. K wa njia moja au nyingine, mifano yote ya Yesu kuhusiana na ufalme (“Ufalme wa Mungu ni kama. . . .”) inatangaza na/au kueleza siri hii. Uelewa huu wa Ufalme ni mpya kabisa. Wayahudi wa Palestina ya karne ya kwanza walihitaji kuusikia ujumbe huu, kuuelewa na kuuamini. Hili ndilo jambo kuu la mahubiri na mafundisho ya Yesu. 14. H ivyo, tunaweza kuelewa fundisho la Yesu kuhusu kuja kwa Ufalme wa Mungu kama jambo la sasa na la wakati ujao pia. Ufalme upo sasa na bado haupo. Yesu anatangaza uwepo wa wakati ujao. 15. T aswira hii ya Ufalme wa Mungu katika mafundisho ya Yesu inaweza kutusaidia kuona kwa uwazi zaidi kile anachosema. Taswira hii ni mpangilio wa nyakati tangu Uumbaji hadi wakati ujao wa milele (wa milele katika Biblia inamaanisha wakati usio na mwisho). a. Wakati wa Ufalme ni wakati ujao. Sasa tunaishi katika enzi hii na ile ijayo. b. Ufalme wa Mungu una vipindi viwili, kila kimoja kina sifa ya kuja kwa Yesu akiwa Mfalme wa Kimasihi ili kuleta utawala wa Mungu. 16. U falme wa Mungu unaleta baraka za Mungu. Watu wa Ufalme wanapoishi sasa katika mvutano wa kuwapo kwa Ufalme na wakati ujao wa Ufalme, baadhi ya baraka tayari zimetufikia na nyingine zinangoja ukamilifu wa Ufalme wakati ujao.
Baraka za Sasa za Ufalme a. Injili inahubiriwa
b. Msamaha wa dhambi c. Roho Mtakatifu anakaa ndani ya watu wa Mungu d. Utakaso umeanza.
Made with FlippingBook - Online catalogs