The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
/ 1 9 9
UFALME WA MUNGU
Ufalme Wako Uje! Usomaji kuhusu Ufalme wa Mungu (muendelezo)
Baraka za Wakati Ujao wa Ufalme a. Uwepo wa Mungu
b. Miili ya ufufuo c. Utakaso kamili d. Shalom : amani, haki, furaha, afya, ukamilifu e. Mbingu mpya na nchi mpya f. Hukumu na uharibifu wa maadui wote wa Mungu ikiwa ni pamoja na dhambi, kifo, shetani na mapepo wake, uovu wote. 17. T usipuuze ukweli ulio wazi kwamba kitendo cha Yesu kuhubiri kuhusu Ufalme kwake ni tangazo kuu kumhusu Mungu. Mungu anauleta Ufalme wake kama Baba anayetafuta, mwenye kukaribisha, na mwenye neema. Pia anakuja akiwa mwamuzi kwa wale wanaoukataa Ufalme wake. 18. U falme wa Mungu ni kazi ya Mungu kabisa. Kwa neema anaingia katika historia ya wanadamu kwa njia ya Mwanawe Yesu Kristo ili kuleta utawala wake duniani. Kwa hiyo Ufalme ni wa kupita fahamu kabisa na wenye neema. Wanadamu hawawezi kuleta, kujenga au kukamilisha Ufalme. Ni tendo la Mungu kabisa. 19. M iujiza ya Yesu na kufukuza pepo ni ishara kwamba Ufalme wa Mungu uko ndani yake na katika huduma yake (Mt. 11:1-6; 4:23; 9:35; 10:7-; Lk 9:1, 2, 6, 11). 20. U falme wa Mungu unauvamia ufalme wa Shetani Yesu anapokuja na kuuleta Ufalme (Mt. 12:22-29; 25:41; Mk. 1:24, 34; Lk 10:17-; 11:17-22). 21. U falme wa Mungu ni wa thamani kuu, hakika ni jambo kuu kuliko yote katika ulimwengu wote (Mt. 13:44-46). Kwa hiyo, ni lazima tuulize, “Tunapaswa kuitikiaje kuhusu Ufalme huu?” au “Tunaipokeaje zawadi hii ya Ufalme wa Mungu?”
Made with FlippingBook - Online catalogs