The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
2 6 2 /
UFALME WA MUNGU
KIAMBATISHO CHA 32 Tamko letu la kutegemea:- Uhuru Katika Kristo Mch. Dkt. Don L. Davis
Ni muhimu kufundisha maadili ya kikristo ndani ya eneo la uhuru ambao tulishindiwa na kifo cha Kristo msalabani na kuingia kwa Roho Mtakatifu katika maisha na utume wa kanisa (Wagalatia 5:1) katika uungwana huo Kristo, alituandikia huru”) na kila wakati katika mazingira ya kutumia uhuru wako katika mfumo wa kuleta utukufu wa Mungu na kuendeleza ufalme wa Kristo pamoja na baadhi ya vifungu pambanuzi juu ya uhuru katika nyaraka, Nina amini tunaweza kuwaandaa wengine kumwishia Kristo na ufalme wake, Kwa kusisitiza kanuni ya “6-8-10” ya 1 wakorintho na kuvitumia katika masuala ya maadili. 1. 1 Kor. 6.9-11- Ukristo ni kuhusu mabadiliko katika Kristo; hakuna kiasi cha udhuru ambao utampeleka mtu ndani ya Ufalme. 2. 1 Kor. 6.12a – Tuko huru katika Kristo, lakini si kila kitu akifanyacho mtu kinafaidia au kinasaidia. 3. 1 Kor. 6.12b – Tuko huru katika Kristo, lakini kitu chochote ukikizoelea na kukitenda hata kukuendesha kinyume na Kristo na ufalme wake. 4. 1 Kor. 8.7-13 – Tuko huru katika Kristo, lakini hatupaswi kujivunia uhuru wetu, hususani mbele ya Wakristo ambao dhamira zao zitaharibiwa na kujikwaa wakituona tukifanya kitu cha kuchukiza. 5. 1 Kor. 10.23 – Tuko huru katika Kristo; kila kitu ni halali kwetu, lakini si kila kitu ni cha kusaidia, wala kufanya kila kitu humjenga mtu 6. 1 Kor. 10.24 – Tuko huru katika Kristo, na tunapaswa kutumia uhuru wetu kuwapenda ndugu na dada zetu katika Kristo na kuwalea kwa ustawi wa watu wengine. (Gal 5.13) 7. 1 Kor. 10.31 – Tuko huru katika Kristo na tumepewa uhuru huo ilituweze kumtukuza Mungu kwa vyote tunavyofanya, iwe tunakula au tunakunywa au chochote tunachofanya. 8. 1 Kor. 10.32-33- Tuko huru katika Kristo, na tunapaswa kutumia uhuru wetu kufanya chochote tunachoweza kufanya kusiwakoseshe watu wa dunia au kanisa, lakini tufanye tunachofanya ili kuwaathiri kumjua na kumpenda Kristo k. m kwamba waweze kuokolewa. Kwa kuongezewa kanuni hizi, ninaamini pia tunapaswa kutilia mkazo kwa kanuni zifuatazo:
Made with FlippingBook - Online catalogs