The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
/ 2 6 3
UFALME WA MUNGU
Tamko letu la kutegemea:- Uhuru Katika Kristo (muendelezo)
• 1 Pet. 2.16 -- Tunapaswa kuishi huru katika Kristo kama watumishi wa Mungu, lakini kamwe tusitafute kutumia uhuru wetu kuficha maovu. • Yohana 8.31-32 – Tunajionyesha kuwa wanafunzi wa Kristo tukitii na kuendelea katika neno lake, na kwa kufanya hivyo tunakuja kujua ukweli, na ukweli unatuweka huru ndani yake. • Gal. 5.13 – Kama ndugu na dada katika Kristo, tunaitwa kuwa huru, bali si kutumia uhuru wetu kama ruhusa ya kuendekeza asili yetu ya dhambi bali tumeitwa kuwa huru ili kutumikiana kwa upendo. Lengo hili juu ya uhuru, akilini mwangu, huweka vitu vyote ambavyo tunawaambia watu wazima au vijana katika mazingira ambamo mambo hutokea mara nyingi, njia ambayo huwafanya wanafunzi wakristo wapya wengi, ni kupitia mipangilio migumu. Kwa kuorodhesha maovu mbali mbali na maadili mabaya, na hii inaweza kwa wakati mwingine, si tu kuwapa fikira kwamba ukristo ni dini ya kutotenda (dini ya kutofanya mambo) na/au ni imani inayohusika sana na kutofanya dhambi. Kwa kweli, lengo na maadili katika ukristo ni juu ya uhuru, uhuru uliopatikana kwa gharama kubwa, Uhuru wa kumpenda Mungu na kuendeleza ufalme, uhuru kuishi maisha yaliyosalimishwa mbele ya Bwana. Wajibu wa maadili wa wakristo wa mjini ni kuishi huru katika Yesu Kristo, kuishi huru kwa utukufu wa Mungu, na si kwa kutumia uhuru wao kutoka katika sheria kuwa kibali kwa ajili ya kutenda dhambi. Kiini cha mafundisho basi, ni kulenga katika uhuru uliopatikana kwa ajili yetu kupitia kifo cha Kristo na kufufuka, na mwungano wetu na yeye. Sasa tumewekwa huru mbali na sheria, kanuni ya dhambi na kifo, hukumu na hatia ya dhambi zetu wenyewe, na uthibitisho wa sheria juu yetu, tunamtumikia Mungu sasa kwa shukrani, na msukumo wa maadili ni kuishi huru katika Kristo. Hata hivyo hatutumii uhuru wetu kuwa welevi au vichwa juu bali kumtukuza Mungu na kuwapenda wengine. Haya ndiyo mazingira yanayopelekea linalokera la ushoga, utoaji mimba, na maovu mengine ya kijamii. Wale wanaojiingiza katika vitendo kama hivyo wanabuni uhuru wao, lakini kwa kukosa maarifa ya Mungu katika kristo, wanafuata tu mwelekeo wao wa ndani ambao hautokani na mapenzi ya Mungu au upendo wake. Uhuru katika Kristo ni bango la wito kuishi kama watakatifu na kwa furaha kama wanafunzi wa mjini. Uhuru huu utawawezesha kuona jinsi wanavyoweza kuwa wabunifu kama wakristo katikati ya wale wanaojiita “maisha huru” ambayo hupelekea kwenye utumwa aibu na majuto.
Made with FlippingBook - Online catalogs