The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

3 4 /

UFALME WA MUNGU

Sasa ni wakati wa wewe kushughulikia maswali yako mwenyewe kupitia majadiliano na wenzako darasani. Katika kutafakari kuhusu somo hili na dhana ulizopitia, ni maswali gani hasa yanayokujia akilini? Labda yafuatayo yanaweza kuibua maswali yako mahususi na muhimu. * Unapaswa kuelewaje maana ya Enzi Kuu ya Mungu katika ulimwengu usio wa haki na usiomcha Mungu? * Je, unahisi ni haki na sahihi kwako kwamba Biblia inafundisha kwamba hali yetu ya sasa ni matokeo ya moja kwa moja ya uasi wa kishetani na wa kibinadamu uliofanywa maelfu ya miaka iliyopita? * Ni dhana gani haileti maana kwako kuhusu matokeo ya Anguko? Je, kuna mapungufu katika uelewa wako wa kosmos , sarx na kakos ? * Je, unatatizika hata kidogo na dhana ya utawala wa Mungu kupingwa? Kwa maneno mengine, ikiwa Mungu ni mweza-yote, kwa nini aliruhusu mtu yeyote, hata Shetani, apinge utawala wake? * Je, Mungu anaweza kuwawajibisha wengine kwa makosa ya watu wengine? Kwa kuwa inaonekana kwamba dhambi na kutotii kwao ni matokeo ya yale ambayo Shetani na Adamu walifanya, si yale waliyofanya wenyewe? Je, hii inawezekanaje? * Je, sisi tunaoamini sasa tunatofautiana kwa kiwango gani na wengine wasiomjua Kristo? Je, bado tuko chini ya udhibiti wa shetani, nguvu za dhambi, na majaribu ya ulimwengu? Ni zana gani, ahadi, baraka, na nyenzo gani ambazo Mungu ametupa ili tuishi chini ya utawala wake leo? Leo, makumi ya maelfu ya vijana wanashiriki katika magenge ya uhalifu ambayo yanaharibu mamia ya vitongoji vya miji kote nchini. Wanaume, wanawake, wavulana, na wasichana wengi wasio na hatia wanaishi kwa hofu ya maisha yao kwa sababu ya shughuli na jitihada za magenge hayo, ambayo mengi yanajihusisha na jeuri, ukatili, na uhalifu. Hata hivyo, kwa wengi wa wale wanaoshiriki katika vikundi hivyo, vikundi hivyo ndio familia pekee ambazo wamewahi kujua. Wanapokea upendo mwingi, heshima, na kujali kwingi kati ya washiriki wa magenge husika na familia zao, ingawa wanapata maumivu mengi pamoja. Katika kuangalia hali ya magenge katika mitaa duni ya majiji, je, theolojia uliyosoma wiki hii inatoa tafsiri gani kwa hali hii? Zaidi ya hilo, je, kuna namna ambazo uhalisia huo wa magenge haujafafanuliwa na mada zinazozungumziwa katika somo la “ Kupingwa Magenge katika Mitaa Duni ya Jiji

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi

1

MIFANO

1

Made with FlippingBook - Online catalogs