The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 4 3

UFALME WA MUNGU

MIFANO YA REJEA

Ungejibuje Swali Lifuatalo?

“Mungu alianza kuzindua (yaani, kuanza) utawala wa ufalme wake maishani mwangu wakati……….” Je, unaweza kukumbuka wakati ambapo Mungu alianza kazi ya ufalme wake katika maisha yako? Je, aliianza siku ulipotubu na kuamini? Siku ambayo ulikuja kuwa mshiriki wa kanisa lako la mahali pamoja? Siku ulipozaliwa kimwili, au kabla ya hapo? Ikiwa ungekisia tarehe ambayo kazi ya ufalme wa Mungu ilianza katika maisha yako, ungesema ni lini?

1

Kweli au Si kweli?

“Ni vyema kusema kwamba Ufalme wa Mungu haujawahi kuwa na mwanzo au uzinduzi wowote, kwa kuwa Mungu amekuwa Mungu siku zote, na kama Mungu, amekuwa akitawala siku zote.” Je, kipi ni sahihi kuhusu kauli hii? Je, kuna chochote hapa ambacho kinaweza kupotosha? Je, utawala wa Mungu katika maisha ya mtu, familia, au taifa una mwanzo, au je, Mungu amekuwa Bwana wa maisha yetu daima, bila kujalisha kwamba tunakiri hivyo au la?

2

2

Utashi

Katika historia yote ya falsafa na theolojia, watu wacha Mungu, wanyoofu wamejadiliana juu ya swali la uhuru wa kuchagua, yaani, je, kweli tuna kitu chochote kama hiari ndani yetu? Fikiria juu ya hilo kwa muda. Ikiwa ungeulizwa, “Je, tuko huru?”, ungesema nini? Sisi kama wanadamu tuko huru kufanya nini? Je, sisi ni watumwa wa dhambi, au watumwa wa Mungu, au tuna chaguo katika kila jambo tunalolifikiria, tunalofanya na tunalokutana nalo? Ikiwa hatuna uhuru wa kuchagua, Mungu anawezaje kutuwajibisha kwa yale tunayosema na kufanya?

3

Made with FlippingBook - Online catalogs