The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

4 2 /

UFALME WA MUNGU

umekuja, yaani, kwamba ulikuwa “umekaribia.” Utawala wa Mungu, ambao ulikuwa umeahidiwa na kutamaniwa, ulikuwa umefika sasa kwa kuja kwa Yesu wa Nazareti ulimwenguni. Pamoja na kuvutia na ukuu wa tangazo hili, ni wachache sana waliolisikia na kulielewa katika uzito na uhalisia wake – kuanzishwa kwa utawala wa Mungu, mwisho wa uasi wa shetani, mwisho wa laana, na ahadi ya maisha mapya katika Ufalme wa Mungu. Ni wachache tu waliouelewa ujumbe ule siku hiyo. Vipi leo? Je, unamsikia Mwana wa Mungu akitangaza leo kwamba “Ufalme wa Mungu umekaribia?” Ushauri wake ni wenye kutoa uhai na wa ajabu leo ​kama ilivyokuwa siku ile kwa watu wa kawaida huko Galilaya; tukimsikia akisema sasa, leo, tunaweza kumrudia Mungu, kugeuka kutoka katika dhambi, na kukumbatia ukweli wa Habari Njema katika Kristo. Tunaweza kuja chini ya utawala wa Mungu ikiwa tu tutaitikia tangazo hili, na kuitikia sauti ya Mwokozi leo. Baada ya kutamka na/au kuimba ukiri huu wa imani (taz. Kiambatisho) omba maombi yafuatayo: Mungu Mwenyezi, kwa kifo cha Mwanao umeiharibu dhambi na mauti, na kwa ufufuo wake umeleta haki, yaani kutokuwa na hatia, na uzima wa milele, ili sisi, tukiwa tumekombolewa kutoka katika nguvu za ibilisi, tukae katika Ufalme wako. Utujalie tuyaamini haya kwa moyo wote na, tukiwa thabiti katika imani, kukusifu na kukushukuru; kwa njia ya Mwanao Yesu Kristo Bwana wetu, Amina. ~ Martin Luther amenukuliwa na Andrew Kosten. Ibada na Maombi ya Martin Luther . Grand Rapids: Baker Book House, 1965. uk. 49.

2

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 1, Kupingwa kwa Utawala wa Mungu .

Jaribio

Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita: Isaya 14:12-17.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukabidhi

Made with FlippingBook - Online catalogs