The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 5 1

UFALME WA MUNGU

Hitimisho

» Tangu mwanzo, Mungu amekusudia kukomesha kutotii na uasi wote ambao ni matokeo ya Anguko. » Mungu alifanya agano na Abramu kama ahadi yake ya dhati ya kumleta Mzao ambaye kupitia kwake ufalme na utawala wa shalom na haki ungerejea duniani. » Israeli ni watu wa agano la Mungu ambao kupitia kwao Masihi angekuja (kupitia Ibrahimu, Mababa, Yuda, na Daudi). Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yaliibuka kutokana na maudhui ya video. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko. 1. Biblia inafafanuaje dhamira ya Mungu ya kuwaweka huru wanadamu kutoka katika utumwa na ubinafsi wa “nyoka”? Je, ni lini Mungu aliamua kutokomeza dalili zote za laana na Anguko? 2. Proto-evangelium ni nini, na kwa nini ni muhimu kwa ufahamu wetu kuhusu Ufalme wa Mungu? 3. Kwa nini ni muhimu kwamba Mungu alitoa ahadi kuhusu Mzao na nyoka mara tu baada ya Anguko? Je, hili linaashiria nini kuhusu nia ya Mungu ya kushinda madhara ya Anguko? 4. Ni kwa jinsi gani mada za Mungu kama Shujaa wa Kiungu na proto evangelium zinahusiana? Je, ni baadhi ya njia gani ambazo Mungu alijidhihirisha katika Agano la Kale kama Shujaa wa Kiungu? 5. Kulingana na Longman na Reid, ni zipi awamu tano za Mungu kama Shujaa wa Kiungu zinazotajwa katika Maandiko? Jukumu la Mungu kama Shujaa wa Kiungu linajidhihirishaje katika uhamisho na utumwa wa Israeli na Yuda? 6. Ni ahadi gani mahususi zilizojumuishwa katika agano la Mungu na Abramu? Agano la Abramu linahusianaje na ahadi ya Mungu katika proto evangelium ?

Segue 1

2

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook - Online catalogs