The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
/ 7 5
UFALME WA MUNGU
2. Siku ya Pentekoste: kumwagwa kwa Roho Mtakatifu (katika utimilifu wa unabii wa Yoeli), Mdo. 2:8.
B. Roho Mtakatifu katika Kanisa ndiye dhamana [arabuni] na kionjo cha baraka kuelekea baraka kamili za Ufalme ujao.
1. Roho kama “arabuni [dhamana] ya urithi wetu,” Efe. 1:13-14
2. Muhuri wa Mungu na Roho Mtakatifu ndani ya mioyo yetu kama dhamana ya ahadi yake ya agano kwa ajili ya ukombozi, 2 Kor. 1:21 22.
3. Matendo makuu ya ufalme na matunda ya Roho juu yetu sasa yanatumika kama kionjo cha baraka kamili ijayo.
3
4. Arrabon : arabuni, malipo ya awali ( advance payment ), ahadi, malipo ya awamu ya kwanza (“dhamana”).
C. Pia, Roho Mtakatifu ndiye Bwana aliye hai, anayetia nguvu, anaongoza na kulielekeza Kanisa.
1. Roho Mtakatifu ni Mungu: Mungu katikati ya watu wa Mungu leo.
2. Kila kanisa la mahali linaye Roho Mtakatifu aliyeahidiwa kwa imani katika Yesu Kristo.
3. Huduma ya Roho Mtakatifu katikati ya mwili, yaani, Kanisa:
a. Anatuongoza katika kweli yote (Yohana 15:26).
Made with FlippingBook - Online catalogs