The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 7 7

UFALME WA MUNGU

2. Ekklesia ya Mungu iliyoitwa iko hapa, 1 Pet. 2:8-9.

3. Pumziko la Sabato ya Mungu sasa linafurahiwa kwa imani katikati ya Kanisa, Ebr. 4:3-10.

4. Baraka za Mwaka wa Yubile zinatekelezwa na kufurahiwa katika mwili, Kol. 1:13.

5. Roho Mtakatifu anakaa ndani ya Kanisa, 2 Kor. 1:20.

6. Nguvu za enzi ijayo na Shetani amelemazwa katikati ya Kanisa, Gal. 3:10-14.

3

7. Shalom ya Mungu (ukamilifu) inashuhudiwa katika Kanisa, Rum. 5:1.

8. Tuna uwezo uokokoao wa Injili ya Kristo, Rum. 10:9-10. Kanisa ni mahali ambapo tunaweza kuja na kupata uzoefu wa nguvu na uwepo wa Roho wa Mungu, na kufurahia faida za utawala wa Mungu juu ya maisha yetu!

B. Ufalme wa Mungu unadhihirishwa katika maisha, ushuhuda, na ushahidi wa kanisa.

1. Kwa Kanisa, Ufalme ni zawadi na kazi.

a. Ufalme ni zawadi: Utawala wa Mungu unapatikana kwa wote wanaomwamini Mwanawe.

Made with FlippingBook - Online catalogs