The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
/ 8 9
UFALME WA MUNGU
* Je, inawezekana mtu kudai kuwa na wokovu katika Kristo huku ukilidharau au kulikataa Kanisa? Je, ni mambo yasiyoweza kutenganishwa – kwa maneno mengine, ikiwa umempata Yesu, ni lazima pia uwe sehemu ya Kanisa? * Je, unafanya nini ikiwa unahudumu kati ya watu ambao hawajawahi kuona Kanisa kama linavyofafanuliwa katika Maandiko? Je, unawasaidiaje watu kupata uzoefu wa Kanisa kwa namna ile Mungu anavyolielezea? * Je, ni sawa kufungamanisha Ufalme kwa ukaribu sana na maisha na afya ya Kanisa? Ni kwa njia gani Ufalme unadhihirishwa tofauti na Kanisa? * Ni kwa kiwango gani tunaweza kutarajia Roho Mtakatifu kuonyesha ishara na maajabu katika huduma zinazowakilishwa hapa, katikati ya makanisa na huduma za wanafunzi wetu? Je, ni masharti gani, kama yapo, ni muhimu kutimiza ili kuona nguvu ya Mungu ikiambatana na huduma yetu ya Neno? * Tunashindaje jeuri, maumivu, na magumu ya jiji tukiwa mawakala wa Ufalme? Inaonekana kana kwamba jiji ni kubwa sana na sisi ni wadogo sana – tunabadilishaje mtazamo wetu kuhusu sisi wenyewe na kile tunachofanya? * Kuna uhusiano gani kati ya uvamizi wa utawala wa Mungu ndani ya jiji na nguvu za giza zinazouweka katika utumwa? Je, tunapaswa kufanya nini ili kufahamu njia mahususi ambazo shetani huwaweka watu wa jiji katika utumwa? * Je, inawezekana kuwa ndani ya Kanisa na bado usiwe chini ya utawala wa Mungu? Ikiwa ndivyo, jinsi gani? * Ni hatua gani zinahitajika ili kuona uamsho ukija kwa kanisa au jumuiya ya Kikristo ambayo haionekani kutoa ushuhuda wenye nguvu juu ya utawala wa Mungu katika maisha na ushuhudiaji wake? * Je, ni nafasi gani ambayo viongozi wanayo katika kuona Kanisa linakuwa eneo na wakala wa Ufalme? * Makanisa yanaweza kujifungia ndani ya mipaka yake na kuishi katika kugawanyika na matengano – unawezaje kuchukua maono ya kibiblia na kuyashirikisha katika makanisa ili kuwapa changamoto ya kuhubiri habari za Ufalme wa Mungu pamoja ?
3
Made with FlippingBook - Online catalogs