The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
9 0 /
UFALME WA MUNGU
MIFANO
Je, Hili ndilo Jambo Halisi?
Hivi majuzi katika kanisa dogo, vijana wamemgeukia Bwana kwa namna ya ajabu. Baada ya miezi kadhaa ya maombi ya muda mrefu na kushirikiana waziwazi kati ya mtu na mwingine, kikundi hiki cha wanafunzi wa shule ya upili wapatao 100 au zaidi walianza kuona Mungu akifanya mambo ya ajabu katikati yao. Mbali na idadi kubwa ya wanafunzi kuwashirikisha marafiki zao imani yao na kuwaona wakija kwa Bwana, idadi ya wanafunzi waliungama dhambi zao mbele za Bwana na mbele za watu, wakikiri matumizi mabaya ya pombe, dawa za kulevya na kufanya ngono haramu. Ibada ya kundi hili ilikuwa ya ajabu – masaa yalionekana kupita bila hisia yoyote ya hasara kwa sababu ya ukubwa, upya, na ukweli wa ibada. Ingawa matokeo ya mabadiliko haya yalionekana kuathiri vijana tu, kanisa zima likapendezwa na kuanza kutazama matokeo ya umwagiko huu mpya na kujiuliza kama ungeenea kwa kanisa zima. Kwa kuzingatia mafundisho tuliyojadili leo darasani, kiongozi wa kikundi cha vijana anapaswa kuwafundisha nini vijana hawa kuhusu hali hii? Wanapaswa kufanya nini kama Wakristo wachanga katika kanisa kubwa, lisilo na ushiriki mzuri wala uhai? Wanawezaje kutumiwa kuwa mashahidi bora zaidi wa Ufalme, ndani na nje ya kanisa lao? Mchungaji kijana wa kanisa dogo la mjini alifanya kazi bila kuchoka akitamani kwa miaka mingi kuona Mungu akitenda kazi ndani ya kanisa, bila mafanikio. Ni kanisa dogo la kimadhehebu, ambalo linafanya kazi kama mtoto wa kambo katika dhehebu kubwa zaidi. Washirika wengi wako kwenye migogoro baina yao, na idadi kubwa imeonyesha kusikitishwa na uongozi wake katika kanisa. Ametafuta vitabu na nyenzo mbali mbali za kisasa kuhusu ukuaji na uhuishaji wa kanisa, lakini hakuna kitu ambacho kimeonekana kufanya kazi. Kusema kweli, amevunjika moyo sana hivi sasa. Anafahamu uelewa wako wa uhusiano kati ya Kanisa na Ufalme. Ungemwambia nini huyu mchungaji kijana wa mjini ili kumtia moyo katika huduma yake? Je, ajiuzulu na atafute kanisa lingine, avumilie humo na washirika wanaoonekana kuwa wachache, wasioridhika? Anawezaje kubadili maoni yake mwenyewe ili kupata moyo na ari mpya anayoihitaji ili kuendelea? Karibu na Kukata Tamaa
1
3
2
Ni nani Hasa Anaudhihirisha Ufalme?
Shemasi mmoja, Bw. Jones, amekuwa na furaha kwa muda wa miezi 12 iliyopita kuhusu huduma ya magereza ambayo imeanza hivi majuzi katika kanisa lake. Takriban watenda kazi 3-4 kila wiki huenda kwenye jela ya eneo la karibu na kutengeneza urafiki na wafungwa, kuwapa mahitaji ya kimwili na kuwashirikisha
3
Made with FlippingBook - Online catalogs