The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 9 1

UFALME WA MUNGU

habari za Kristo. Matokeo yamekuwa ya ajabu! Zaidi ya wanaume na wanawake 20 wamempokea Kristo, na hivi karibuni wengi wao watatimiza vigezo vya kuondoka ili kutumikia kifungo cha nje ikiwa si kuondoka moja kwa moja kutoka katika mfumo wa magereza. Bwana Jones ameenda kwa mchungaji akipendekeza kwamba kanisa litengeneze mpango wa kuwaleta waamini hawa wapya katika kanisa lao, kuwafanya kuwa wanafunzi na kufanya kazi nao ili kuwafanya warejee kwa ufanisi katika jamii. Mchungaji amepokea simu kutoka kwa washirika wenye wasiwasi kwamba mmiminiko mkubwa wa wafungwa unaweza kusababisha machafuko katika kanisa, “na zaidi ya hayo, wengi wa watu hawa wamefanya mambo ya kutisha. Je, tuweke watoto wa washirika wetu kanisani katika mazingira ya pamoja na watu wa aina hii?” Bwana Jones amekuomba ushauri. Kwa kuzingatia yale unayojua kuhusu Kanisa, Ufalme, na huduma ya mjini, ungependekeza nini yeye, mchungaji, na kanisa wafanye ili kufaidika na fursa hii huku wakizingatia maoni ya washirika? Kanisa la Yesu Kristo, kama mwili na wakala wake, lenyewe ndilo kituo (mahali na/au muktadha) wa wokovu wa Mungu, wa uwepo wa Roho Mtakatifu wenye kutia nguvu, na wa madhihirisho halisi ya maisha na ushuhuda wa Ufalme. Kanisa la Yesu Kristo sio tu mahali, bali pia ni wakala wa Mungu, mtumishi wa Mungu aliye tayari na anayepatikana ili kuendeleza makusudi ya ufalme duniani kama Kanisa Pambanaji katika enzi hii ya sasa. Ikiwa una nia ya kusoma zaidi kuhusu Kanisa la Yesu Kristo kama mahali na wakala wa Ufalme wa Mungu katika ulimwengu wa sasa, unaweza kujaribu vitabu hivi: Perkins, John. With Justice for All . Ventura: Regal Books, 1984. Sider, Ron. Rich Christians in an Age of Hunger . Downers Grove: InterVarsity Press, 1977. Snyder, Howard A. The Community of the King . Downers Grove: InterVarsity Press, 1977. Stott, John W. Involvement: Being a Responsible Christian in a Non-Christian Society . Toleo la 1. Old Tappan: Fleming H. Revell Co., 1985.

Marudio ya Tasnifu ya Somo

3

Nyenzo na Bibliografia

Made with FlippingBook - Online catalogs