The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
/ 9 9
UFALME WA MUNGU
tafadhali mpe mwalimu wako mapendekezo yako ya Kazi ya Huduma, pamoja na kifungu ulichochagua kwa ajili ya Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko.
MIFANO YA REJEA
Mambo Mengi Pasina Sababu
Katika kujadili mfululizo wa hivi punde wa mahubiri ambayo mchungaji wao amekuwa akihubiri juu ya mada ya nyakati za mwisho, wanandoa fulani walijadili kama mahubiri kama hayo yalikuwa ya manufaa kwa kanisa au la, na kwa ukuaji wa Wakristo ndani yake. Ilionekana kana kwamba mchungaji alikuwa akikazia fikra mambo mengi ya neno la unabii, na wengi wa wasikilizaji walikuwa wakichanganywa na nadharia mbalimbali alizokuwa akizungumzia kuhusu unyakuo, dhiki kuu, ziwa la moto, na mambo mengine, ambayo yote yalionekana kuwa mbali sana na mapambano yao ya kila siku wakiwa walimu katika shule ya upili ya eneo hilo. Baada ya mazungumzo mengi, walikubaliana kwamba masomo kama hayo, ingawa yanafaa kwa mseminari au kwa viongozi wa kanisa, si ya maana sana kwa maisha ya Kikristo kwa “Wakristo wa kawaida.” Unakubaliana na uchambuzi wao? Kwa nini ndio au kwa nini hapana? Unafikiri nini kuhusu wazo ambalo limekuwa maarufu kuhusu hukumu ya mwisho ya Mungu juu ya dhambi, hasa miongoni mwa madhehebu kama vile Mashahidi wa Yehova, wanaosema kwamba Mungu mwema na mwenye upendo hangeweza kudai adhabu ya milele kwa wale waliovunja sheria yake? Je, inaonekana kuwa jambo la busara au lisilo na akili kwako kutazamia kwamba Mungu angehitaji malipo ya milele kutoka kwa wale wanaokosa kutubu na kumwamini Yesu Kristo? Je, hii haionekani kuwa jambo la kupita kiasi – je, kuna mtu yeyote duniani ambaye kwa kweli amekuwa mbaya kiasi cha kustahili adhabu ya milele kutoka kwa Mungu? Ungeanzaje kusuluhisha maswali kama haya, ikiwa utakabiliwa nayo? Fikia Mambo Muhimu Kwanza Katika kujadili orodha inayofuata ya masomo ambayo wangefundisha kwa vijana wao katika darasa lao la uanafunzi, vijana wawili waajiriwa wa mjini walitofautiana kuhusu hitaji la kuwafundisha wanafunzi wao juu ya “mambo ya mwisho.” Kwa kuwa katika miaka mitano waliyoongoza vijana hawakusema neno lolote kuhusu mambo haya, mmoja wa viongozi alifikiri kwamba wanapaswa kufanya hivyo. Mungu Mwema Hawezi Kudai Kitu Kama Hicho
1
4
2
3
Made with FlippingBook - Online catalogs