Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika moduli ya Theolojia ya Kanisa , utahitajika kufanya ufafanuzi (uchambuzi wa kina) wa mojawapo ya vifungu vifuatavyo vya Neno la Mungu:  Warumi 12:3-8  Wagalatia 3:22-29  1 Wakorintho 12:1-27  Waefeso 2:11-22  Waefeso 4:1-16  1 Petro 2:9-10 Madhumuni ya kazi hii ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa andiko mojawapo muhimu kuhusu Kanisa. Unaposoma kwa kina, kutafakari, na kujifunza juu ya mojawapo ya vifungu hivi, matumaini yetu ni kwamba utaweza kuelewa na pia kuonyesha jinsi kifungu hiki kinavyoangazia au kuweka wazi kipengele fulani cha maono ya Mungu kwa watu wake. Na bila shaka, katika kulielewa Kanisa vyema, maombi yetu ni kwamba utakuwa na ufanisi zaidi katika kuhusianisha kweli hizi na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, uongozi wako katika kanisa lako, na huduma yako mjini. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia , ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika? 2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo? Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)

Dhumuni

Mpangilio na Muundo

Made with FlippingBook - Share PDF online