Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
Mwongozo wa Mkufunzi
Theolojia ya Kanisa Kanisa la Mwenyezi Mungu katika Yesu Kristo ni mojawapo ya mada zenye kuburudisha na muhimu zaidi katika Maandiko yote. Yesu wa Nazareti, kupitia kifo chake, kuzikwa, na ufufuo wake, ameinuliwa kuwa kichwa juu ya watu wake wapya, wale walioitwa kumwakilisha duniani na kutoa ushahidi wa Ufalme wake ambao tayari upo japo haujakamilika bado. Kuelewa jukumu la Kanisa katika mpango wa ufalme wa Mungu ni muhimu kwa kila eneo la maisha ya ufuasi wa kibinafsi na wa kusanyiko; hakuna ufuasi au wokovu mbali na tendo la Mungu la kuokoa kupitia Kanisa. Kufahamu kile ambacho Mungu anafanya ndani ya na kupitia watu wake kunampa kiongozi wa watu wa Mungu uwezo wa kumwakilisha kwa hekima na heshima. Kanisa limefunuliwa kwa namna ya kivuli katika kusudi kuu la Mungu la kujiletea utukufu kwa kuokoa jamii mpya ya wanadamu kupitia agano lake na Ibrahimu. Kupitia ibada, ushuhuda, na matendo mema, Kanisa katika vizazi vyote huonyesha sifa ya umoja, utakatifu, ukatoliki (yaani kwamba kanisa ni la ulimwengu mzima), na utume wa ushirika wake. Katika Kanisa, Mungu anaonyesha maisha ya ufalme wake na kutangaza fursa ya neema yake kwa ulimwengu.
Mchungaji Dkt. Don L. Davis , (Ph.D., Chuo Kikuu cha Iowa) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry , ambayo ni huduma ya World Impact . Pia anahudumu kama Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact . TUMI imejizatiti kuwezesha vuguvugu za upandaji makanisa kote ulimwenguni ambazo zinawaandaa viongozi ili kuendeleza Ufalme miongoni mwa watu maskini wa mijini. World Impact ni shirika la kimisheni la Kikristo ambalo limejidhatiti kuwezesha harakati za upandaji makanisa kwa njia ya kufanya uinjilisti, kuandaa na kuwawezesha maskini katika miji ya Amerika. Maono yetu ni kusajili, kuwezesha, na kuwatuma viongozi wa mijini ambao watapanda makanisa na kuzindua harakati za upandaji makanisa ya kienyeji. Rev. Terry Cornett , (Master of Arts, Master of Arts in Religion) served as the Academic Dean of The Urban Ministry Institute. Terry holds degrees from the University of Texas at Austin, the Wheaton College Graduate School, and the C.P. Haggard School of Theology at Azusa Pacific University.
www.worldimpact.org • www.tumi.org
Made with FlippingBook - Share PDF online