Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 3 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

A. Kwanza, tunapigana kama askari wa Mungu kwa kutangaza kweli ya Mungu katika Kristo.

1. Tumeitwa kufichua uongo na dhana potofu za adui popote zinapopatikana. Asili ya vita vya kiroho imejengwa katika kweli ya Mungu, Rum. 3:4.

a. Silaha kuu za ibilisi ni uongo na udanganyifu, Yohana 8:44.

b. Zaidi ya hayo, Ibilisi kwa njia ya mashtaka ya uongo na hila hudanganya ulimwengu mzima, ambao uko chini ya udhibiti wake wenye mipaka, na uliojaa dhuluma, 1 Yoh 5:19.

c. Na katika Ufunuo 12:9-10, tunaona kwamba shetani ndiye mdanganyifu mkuu na mshitaki wa ulimwengu wote.

4

2. Kanisa linatangaza ushindi wa Yesu Kristo, kwa kutangaza bila aibu ushindi uliopatikana kupitia kifo cha Yesu msalabani.

a. Yesu alishinda falme na mamlaka kupitia kifo chake msalabani, Kol. 2:15.

b. Tunatangaza ushindi wa Mungu katika Yesu Kristo, 1 Kor. 15:57-58.

c. Tunamtangaza Yesu Kristo kuwa Bwana, Yeye ambaye jina lake liko juu ya majina yote, ambaye lazima atawale mpaka maadui wote wawekwe chini ya miguu yake, 2 Kor. 4:3-5.

Made with FlippingBook - Share PDF online