Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 1 8 3

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

2. Kushiriki katika jamii mpya ya watu waliochaguliwa na Mungu (1 Pet. 2:9-10). a. Viungo vya mwili wa Kristo (1 Kor. 10:16-17; 12:27). b. Kondoo wa kundi la Mungu chini ya Mchungaji mmoja (Yoh. 10; Ebr. 13:20; 1 Pet. 5:2-4). c. Washiriki wa familia na nyumba ya Mungu (Gal. 6:10; 1 Tim. 3:15). d. Wana wa Ibrahimu na warithi wa ahadi ya agano (Rum. 4:16; Gal. 3:29; Efe. 2:12). e. Wenyeji wa Yerusalemu Mpya (Flp. 3:20; Ufu. 3:12). f. Malimbuko ya Ufalme wa Mungu (Lk 12:32; Yak. 1:18). 3. Uhuru (Gal. 5:1, 13) a. Kuitwa kutoka katika utawala wa giza unaokandamiza uhuru (Kol. 1:13-14). b. Kuitwa mbali na dhambi ambayo ni utumwa (Yoh. 8:34-36). c. Kuitwa kuwa wa Mungu Baba ambaye ni Mkombozi wa watu wake (Kut. 6:6). d. Kuitwa kuwa wa Mungu Mwana ambaye anatoa kweli inayoweka huru (Yoh. 8:31-36). e. Kuitwa kuwa wa Mungu Roho ambaye uwepo wake unaleta uhuru (2 Kor. 3:17).

II. Jamii ya Imani

A. Kanisa ni jamii ya imani, ambayo, kwa imani, imemkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi. Imani inarejelea yote mawili, yaani yaliyomo katika imani yetu na kitendo chenyewe cha kuamini . Yesu ndiye mlengwa (maudhui) ya imani yetu na maisha yake yanapokelewa kwa njia ya imani (imani yetu) kwake na kwa Neno lake. Katika maana hizi zote mbili, Kanisa ni jamii ya imani.

Made with FlippingBook - Share PDF online