Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 1 8 5
THEOLOJIA YA KANISA
Theolojia ya Kanisa (muendelezo)
njia ya kuielewa kikamilifu zaidi na kuitendea kazi Kweli ( Zab. 119:97-99; 1 Tim. 4:16; 2 Tim. 2:15). 4. Kanisa linafanya kazi kama jamii sikivu ambayo inatambua uwepo wa Roho Mtakatifu na inamtegemea ili kutafsiri na kutumia Maandiko kwa ajili ya wakati huu (Yoh. 14:25-26).
D. Kanisa linashindania imani ambayo ilikabidhiwa mara moja tu kwa watakatifu (Yuda 3).
III. Jamii ya Mashahidi
A. Kanisa linashuhudia ukweli kwamba katika kufanyika mwili kwa Yesu Kristo, maisha yake, mafundisho yake, kifo chake na ufufuo wake, Ufalme wa Mungu umekuja (Mk. 1:15; Lk. 4:43; 6:20; 11:20; Mdo. 1:3; 28:23; 1 Kor. 4:20; Kol. 1:12-13). 1. Kanisa linamtangaza Yesu kama Kristo Mshindi ambaye utawala wake utafanya yafuatayo: a. Kuondoa laana juu ya uumbaji na wanadamu (Ufu. 22:3). b. Kumshinda Shetani na mawakala wa mamlaka yake na kuharibu kazi zao (1 Yohana 3:8). c. Kubadili mfumo na mwenendo wa sasa kwa kuwatetea na kuwatunza wapole, wanyenyekevu, waliodharauliwa, wanyonge, wenye haki, wenye njaa na waliokataliwa (Luka 1:46-55; 4:18-19; 6:20-22). d. Kufidia hasira ya haki ya Mungu (Gal. 3:10-14; 1 Yoh. 2:1-2). e. Kuunda jamii mpya ya wanadamu (1 Kor. 15:45-49; Efe. 2:15; Ufu: 5:9-10). f. Kumwangamiza adui wa mwisho – mauti (1Kor. 15:26). 2. Hatimaye, Ufalme wenyewe utakabidhiwa kwa Mungu Baba, na uhuru, ukamilifu, na uadilifu wa Bwana utaenea katika ulimwengu wote (Isa. 10:2-7; 11:1-9; 53:5; Mika 4:1-3; 6:8; Mt. 6:33; 23:23; Luka 4:18-19; Yoh. 8:34-36; 1Kor. 15:28; Ufu. 21).
Made with FlippingBook - Share PDF online