Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 9 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

D. Agano hili linatufungamanisha na wale waliotutangulia. 1. Linatambua kwamba Kanisa ni moja (Efe. 4:4-5). 2. Linatukumbusha kwamba tumezungukwa na wingu la mashahidi ambao wameshiriki katika agano moja nasi (Ebr. 12:1). 3. Linatukumbusha kwamba sisi ni sehemu ya mnyororo mtakatifu: Mungu-Kristo-Mitume-Kanisa. 4. Linatukumbusha kwamba tunashiriki: a. Uzao wa kiroho mmoja (Yoh. 1:13; 3:5-6; 2 Kor. 1:2; Gal. 4:6; 1 Yoh. 3:9). b. Mfanano mmoja wa kifamilia (Efe. 3:15; Ebr. 2:11). c. Bwana mmoja, Imani moja na ubatizo mmoja (Efe. 4:5). d. Roho mmoja anayeishi ndani yetu (Yoh. 14:17; Rum. 8:9; 2 Kor. 1:22). e. Wito na utume mmoja (Efe. 4:1; Ebr. 3:1; 2 Pet. 1:10). f. Tumaini moja na hatma moja (Gal. 5:5; Efe. 1:18; Efe. 4:4; Kol. 1:5). 5. Linatufanya tuelewe kwamba kwa vile tunashiriki agano lile lile, linalosimamiwa na Bwana yeye yule, chini ya uongozi wa Roho yule yule pamoja na Wakristo ambao wametangulia kabla yetu, ni lazima tutafakari juu ya kanuni za imani, mitaguso na matendo ya Kanisa katika historia yote ili kuelewa mapokeo ya kitume na kazi inayoendelea ya Roho Mtakatifu (1Kor. 11:16).

VI. Jamii ya Uwepo

A. “Alipo Yesu Kristo, ndipo lilipo Kanisa” - Ignatius wa Antiokia (Mt. 18:20).

Made with FlippingBook - Share PDF online