Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
1 9 4 /
THEOLOJIA YA KANISA
Theolojia ya Kanisa (muendelezo)
E. Kanisa ni Ukuhani wa kifalme ambao unasimama katika uwepo wa Mungu (1 Pet. 2:5, 9): 1. Kuhudumu mbele za Bwana (Zab. 43:4; Zab. 134:1-2). 2. Kuweka baraka za Mungu juu ya watu wake (Hes. 6:22-27; 2 Kor. 13:14). 3. Kuwaleta watu mbele za macho ya Mungu (1 The.1:3; 2 Tim. 1:3). 4. Kujitoa wenyewe na matunda ya huduma yao kwa Mungu (Isa. 66:20, Rum. 12:1; 15:16). F. Kanisa linaishi katika uwepo wa Mungu kwa njia ya maombi. 1. Maombi kama njia ya kufikia Patakatifu pa Patakatifu (Ufu. 5:8). 2. Maombi kama ushirika na Mungu (Zab. 5:3; Rum. 8:26-27). 3. Maombi kama maombezi. a. Kwa ajili ya ulimwengu (1 Tim. 2:1-2). b. Kwa ajili ya watakatifu (Efe. 6:18-20, 1 The.5:25). 4. Maombi kama shukrani (Flp. 4:6; Kol. 1:3). 5. Maombi kama vita vya Ufalme. a. Kufunga na kufungua (Mt. 16:19). b. Kuzikabili falme na mamlaka (Efe. 6:12,18).
Kanisa ni Jamii Takatifu Ambamo Nidhamu Inafuatwa Ipasavyo
VII. Jamii ya Upatanisho
A. Kanisa ni jamii iliyopatanishwa na Mungu: upatanisho wowote hatimaye unategemea matendo ya Mungu ya upatanisho kwa wanadamu.
Made with FlippingBook - Share PDF online