Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 1 9 7
THEOLOJIA YA KANISA
Theolojia ya Kanisa (muendelezo)
B. Jamii ya Kanisa inamfanania Kristo katika mateso yake. 1. Kwa sababu yanasafisha dhambi (1 Pet. 4:1-2). 2. Kwa sababu yanafundisha utii (Ebr. 5:8). 3. Kwa sababu yanawawezesha watu kumjua Kristo kikamilifu zaidi (Flp. 3:10). 4. Kwa sababu wale wanaoshiriki mateso ya Kristo pia watashiriki faraja na utukufu wake (Rum. 8:17-18; 2 Kor. 1:5; 1 Pet. 5:1). C. Jamii ya Kanisa inateseka kwa sababu inajihusisha na wale wanaoteseka. 1. Mwili wa Kristo huteseka wakati mmoja wa viungo vyake anapoteseka (1Kor. 12:26). 2. Mwili wa Kristo unateseka kwa sababu unajihusisha kwa hiari na watu waliodharauliwa, waliokataliwa, waliokandamizwa na wasiopendwa (Mit. 29:7; Lk. 7:34; Lk. 15:1-2). D. Msalaba wa Kristo ni chombo cha wokovu na kielelezo cha maisha ya Kikristo. Msalaba ni sehemu ya tunu za jamii ya Kanisa. 1. Msalaba wa Kristo ni ishara ya msingi zaidi ya Kikristo. Inatumika kama ukumbusho wa mara kwa mara kwamba Kanisa ni jamii ya mateso. 2. Kigezo cha msingi cha uanafunzi ni utayari wa kuchukua msalaba kila siku na kumfuata Yesu (Mk. 8:34; Lk. 9:23; Lk. 14:27).
IX. Jamii ya Kazi
A. “Kazi za Utumishi” ni alama mahususi ya makusanyiko ya Kikristo wanapotenda haki, kupenda rehema, na kutembea kwa unyenyekevu mbele za Mungu. 1. Uongozi wa Kanisa una jukumu la kuwakamilisha watu wa Mungu kwa ajili ya “kazi za huduma” (Efe. 4:12).
Made with FlippingBook - Share PDF online