Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
3 6 /
THEOLOJIA YA KANISA
Maswali haya yamebuniwa ili kukusaidia kupitia maudhui ya sehemu ya pili ya video inayohusiana na maana ya wokovu. Unapojibu maswali haya, zingatia mawazo yanayofafanua wazi maana ya “wokovu” kulingana na Biblia. Kumbuka kuwa maswali haya hayalengi kufafanua jinsi Yesu alivyotekeleza wokovu au jinsi watu wanavyookolewa (mawazo hayo yatajadiliwa katika moduli nyingine za Capstone), bali yanakusudia kutufanya tuelewe wazi wokovu ni nini. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na pale inapowezekana, tumia maandiko ya Biblia kama uthibitisho! 1. Ni matokeo gani matatu ya dhambi ambayo wanadamu wanahitaji kuokolewa nayo? 2. Mifano ya Yesu kuhusu vitu vilivyopotea katika Luka 15 inatufundisha nini kuhusu wokovu? 3. Kwa nini “kuunganishwa na Kristo” ndio msingi wa wokovu? 4. Kwa nini ni muhimu kuelewa kuwa wokovu daima unahusisha kuingizwa katika Kanisa? 5. Kwa nini muumini Mkristo anaweza kusema “Nimeokolewa” na “Nitaokolewa” na kuelewa kuwa kauli zote mbili zina ukweli unaolingana? Somo hili linazingatia mpango mkuu wa Mungu wa kuwakomboa watu kutoka duniani ili wawe wake milele. Kanisa lilitabiriwa katika agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu, katika siri ambayo imefunuliwa sasa kuhusu mataifa, na kupitia mfano wa watu wa Israeli. Mungu anawaokoa watu wake kwa ajili ya utukufu wake, akiwaunganisha na nafsi yake kwa njia ya imani yao katika Yesu Kristo. Kuokolewa kibinafsi ni kuunganishwa na Kristo kwa imani, na ndani yake, kuunganishwa na jamii yake iliyokombolewa. ³ Kusudi kuu la Mungu, nia yake ya juu kabisa, ni kuleta utukufu na heshima kwake mwenyewe kupitia uumbaji wake na kupitia watu wake ndani ya Yesu Kristo. Vitu vyote vipo kwa mapenzi yake na kwa utukufu wake. ³ Kanisa la Yesu Kristo lilitabiriwa katika tangazo la Mungu kuhusu kusudi lake kuu. Tangu mwanzo, Mungu alikusudia kujiletea utukufu kwa kuwakomboa kutoka kwa wanadamu watu ambao watakuwa wake milele. Alitimiza hili kupitia agano lake na Ibrahimu.
Sehemu ya 2
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
1
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Muhimu
ukurasa 225 15
Made with FlippingBook - Share PDF online