Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 3 9

THEOLOJIA YA KANISA

MIFANO

“Israeli si Watu wa Mungu Tena.”

Hivi karibuni, katika darasa la Shule ya Jumapili la watu wazima lililohudhuriwa na watu wengi, baadhi ya washiriki walihusika katika mjadala mkali kuhusu hadhi ya Israeli katika kazi ya Mungu. Wengine walidai kuwa kwa sababu Wayahudi walihusika katika kifo cha Yesu, hawakubaliwi tena na Mungu kama watu wake. Wengine walisema kuwa ingawa Mungu hajaiacha Israeli kama watu wake, hawana tena nafasi ya upendeleo waliyokuwa nayo hapo awali kwa sababu walishindwa kumwamini Kristo. Kikundi kingine kidogo kilisisitiza kuwa Israeli bado ni watu wa Mungu na wataonekana kuwa hivyo Yesu atakaporudi kwa Mara ya Pili. Kikundi kingine kilisema kuwa suala hilo halina umuhimu hata kidogo, wakisisitiza kuwa tusihangaike sana kuhusu Israeli, bali tumzingatie Kristo na kuokolewa kwa imani ndani yake. Mwalimu akija kwako kutafuta ushauri, utamshauri nini?

1

ukurasa 226  17

1

“Nani Anahitaji Kanisa?”

Rafiki yako anadai kuwa ni Mkristo mwaminifu anayempenda Mungu, anasoma Biblia, na anajitahidi kuishi maisha yenye matendo mema. Hata hivyo, mtu huyu hahudhurii kanisani wala kushiriki katika maisha ya mwili wa Kristo. Kila unapomwalika kanisani, anasema, “Siamini kwamba unahitaji kuwa sehemu ya kanisa ili kuwa Mkristo, zaidi ya hayo, ninamwabudu Mungu vizuri zaidi nikiwa nje kwenye mazingira ya asili kuliko ndani ya jengo la kanisa.” Ungeweza kumwambia nini kuhusu mtazamo wake wa Ukristo?

2

Kuhubiri Biblia Nzima

Kichwa cha somo “Ufunuo Kivuli wa Kanisa” kinaonyesha kwamba kuna uhusiano kati ya watu wa Mungu wa Agano la Kale na Kanisa, wazo ambalo Mtume Paulo analifafanua katika kitabu cha 1 Wakorintho 10:1-11: «Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na

3

Made with FlippingBook - Share PDF online