Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 4 5

THEOLOJIA YA KANISA

Kanisa katika Ibada

SOMO LA 2

ukurasa 229  1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kutetea wazo la kwamba wokovu unakuja kwa neema ya Mungu pekee na kwamba wanadamu hawawezi kuupata kwa kuustahili au kwa jitihada zao binafsi. • Kutambua kwamba ibada ni mwitikio sahihi kwa neema ya Mungu. • Kueleza tofauti kati ya maneno “sakramenti” na “maagizo” na kuelezea mtazamo wa kitheolojia ulio nyuma ya kila neno. • Kuelewa maana ya ubatizo na Meza ya Bwana na kujadili tofauti kuu za namna Wakristo wanavyofikiri kuhusu maana zake. • Kukariri kusudi la msingi la ibada ya Kanisa kwa Mungu: kumtukuza Mungu kwa sababu ya utakatifu wake wa pekee, uzuri wake usio na kikomo, utukufu wake usio na kifani, na kazi zake zisizoweza kulinganishwa na chochote. • Kufafanua kwamba Kanisa linamwabudu Mungu wa Utatu kupitia Yesu Kristo. Tunamwabudu Yehova Mungu pekee, kupitia Yesu Kristo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. • Kujua na kuweka katika vitendo namna Kanisa linavyoabudu kwa njia ya sifa na shukrani, kwa njia ya liturujia ambayo inasisitiza Neno na sakramenti, na kupitia utii na mtindo wetu wa maisha kama jumuiya ya agano.

Malengo ya Somo

2

Tunaleta Dhabihu za Sifa

Ibada

Soma Warumi 12:1-2 , Waebrania 13:15 , na Habakuki 3:17-19 . Moja ya dhana za kawaida zinazohusiana na mfumo wa ibada za Agano la Kale ni dhana ya dhabihu. Katika ibada ya jumla ya hadhara, kama ilivyoungamanishwa na huduma za hekaluni, wale wanaomkaribia Mungu katika namna hizo zote, walitakiwa kutoa dhabihu, iwe katika nyakati za kawaida za ibada, au hasa katika matukio muhimu kama vile kuwekwa wakfu kwa hekalu. Kwenye wakati huu muhimu, damu ya wanyama ilimwagika sana wakati waabudu wakionyesha shukrani zao

ukurasa 230  2

Made with FlippingBook - Share PDF online