Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
5 8 /
THEOLOJIA YA KANISA
a. Mt. 26:26
b. Yn. 6:53-60
Kwa muujiza wa mikate na samaki na kutembea juu ya maji, siku iliyotangulia, Kristo hakuwaandaa tu wasikilizaji wake kwa ajili ya hotuba tukufu [ya Yohana 6] yenye ahadi ya Ekaristi, lakini pia aliwathibitishia kwamba yeye kama Mwenyezi Mungu na mtu, alikuwa na uwezo ulio juu na usio zuiwa na kanuni za asili, na kwa sababu hiyo, angeweza kutoa chakula hicho kisicho cha kawaida, si kingine, zaidi ya Mwili na Damu yake mwenyewe. ~ Joseph Pohle. “Eucharist.” Readings in Christian Theology . Vol. 3. Millard Erickson, mh. Grand Rapids: Baker, 1973. 2. Muungano ni imani kwamba mkate na divai vinakuwa mwili na damu halisi ya Yesu bila kukoma kuwa mkate na divai. Huu ndio mtazamo wa Meza ya Bwana unaoshikiliwa na makanisa ya Kilutheri. Mtazamo huu unakubali wazo la msingi lililojadiliwa hapo juu kwamba mwili halisi na damu ya Yesu viko katika mkate na divai lakini una maelezo tofauti ya jinsi vinavyokuwepo pamoja. 3. Mtazamo wa tatu ni mtazamo wa Matengenezo . Makanisa ya KiPresbiteri na ya Reformed hufundisha kwamba mwili na damu ya Kristo hutolewa kwetu katika Karamu, sio kimwili, lakini kiroho kupitia nguvu na uwepo wa Roho Mtakatifu. Mapokeo haya yanaonyesha kwamba katika kifungu cha Yohana 6 ambacho Yesu anafundisha kuhusu kula mwili wake, anaendelea kusisitiza jambo hili kama kweli ya kiroho: Yn. 6:60-63 – Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema,, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia? 61 Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza? 62 Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza? 63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
2
ukurasa 236 18
Made with FlippingBook - Share PDF online