Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
6 /
THEOLOJIA YA KANISA
kulinganishwa na chochote. Kwa kumkaribia Mungu wa Utatu kwa njia ya Yesu Kristo, Kanisa linaabudu kwa njia ya sifa na shukrani, na kwa njia ya Liturujia inayojikita katika mkazo wa Neno na Sakramenti. Kanisa pia humwabudu Mungu kupitia utii wake na mtindo wa maisha kama jumuiya ya agano. Somo la tatu linaitwa Kanisa kama Shahidi , na linaangazia utume wa Kanisa. Katika somo hili tutashughulikia vipengele muhimu zaidi vya fundisho la uteule jinsi linavyotumika kuhusiana na Yesu Kristo kama mteule wa Mungu, kuhusiana watu wake wateule Israeli na Kanisa, na kuhusiana na waamini binafsi. Tutamwona Yesu Kristo kama Mteule wa Mungu, Yule ambaye kupitia kwake Mungu anaokoa watu kutoka katika ulimwengu kwa ajili yake mwenyewe, na kuchunguza kwa ufupi vipengele na ufafanuzi wa dhana ya watu waliochaguliwa na Mungu kama inavyofafanuliwa kupitia Israeli kama watu wa Mungu na kupitia Kanisa la Yesu Kristo. Kanisa kama chombo cha Mungu cha Utume wake Mkuu, tutaona vipengele vitatu muhimu ndani yake: Kanisa linatoa ushahidi linapowahubiria waliopotea, linapobatiza waamini wapya katika Kristo, yaani, kuwajumuisha kama washiriki katika Kanisa, na linapowafundisha washirika wake kushika mambo yote ambayo Kristo aliamuru. Hatimaye, katika somo la nne, Kanisa katika Kazi , tutaona vipengele mbalimbali vya Kanisa. Tutaangazia kipekee jinsi tunavyoweza kugundua kusanyiko halisi la Kikristo kwa kuzingatia vigezo fulani ambavyo vimethibitishwa kuwa ishara za kweli za matendo na mtindo wa maisha wa Kanisa. Tutazingatia alama za Kanisa kulingana na Kanuni ya Imani ya Nikea, na vile vile kulingana na mafundisho ya Vuguvugu la Matengenezo. Pia tutalitazama Kanisa kwa msingi wa Kanuni ya Vincent, ambayo ni mwongozo muhimu wa kuelewa na kutathmini mapokeo na mafundisho yanayodai kuwa ya lazima kwa Wakristo. Tutamalizia kozi hii kwa kukazia huduma ya Kanisa kupitia taswira mbalimbali za Kanisa zilizotajwa katika Agano Jipya, taswira ya nyumba ya Mungu (familia ya Mungu), kupitia taswira ya mwili wa Kristo na Hekalu la Roho Mtakatifu (wakala wa Ufalme wa Mungu). Pia tutaangalia kupitia dhana ya Jeshi la Mungu jinsi Kanisa linavyopigana katika vita vya Mwana-Kondoo. Taswira hizi zinatoa ufahamu mkubwa wa jinsi tunavyopaswa kuuelewa utambulisho wa Kanisa na kazi yake ulimwenguni leo. Bila shaka, Kanisa la Yesu Kristo ni wakala wa Mungu kwa ajili ya Ufalme wake, na watu wa uwepo wake. Kujifunza kwako moduli hii na Neno la Mungu kuzae ndani yako upendo wa kina kwa watakatifu wa Mungu na kujitoa kwa dhati kuishi kwa ajili ya kulijenga Kanisa! Mungu akubariki sana unapojifunza Neno lake Takatifu kwa bidii!
~Mchungaji Dr. Don L. Davis
Made with FlippingBook - Share PDF online