Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

6 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

3. Hatumwendei Mungu kwa haki na kustahili kwetu wenyewe. Badala yake tunamwendea kupitia huduma ya ukuhani mkuu wa Yesu, tunaweza sasa kumkaribia Mungu wetu mtakatifu tukiwa na uhakika kamili wa imani, Ebr. 10:21-22.

G. Tukiwa tumewekwa huru ndani ya Yesu, tumepewa Roho Mtakatifu ili atupe uwezo wa kuleta ibada inayokubalika kwa Mungu.

1. Kwanza, Roho hutufanya wahudumu wa agano jipya, agano la imani katika Yesu na si katika matendo ya Sheria, 2 Kor. 3:4-6.

2

2. Tunapojazwa na Roho, kusanyiko la waamini linajaa ibada na sifa za juu za Mungu, Efe. 5:18-20.

II. Jinsi Kanisa Linavyofanya Ibada kwa Mungu

ukurasa 238  21

A. Kupitia huduma zetu na mtindo wa maisha wa Sifa na Shukrani. Kulingana na kielelezo cha watu wa Mungu Israeli, Kanisa linahimizwa kusherehekea katika kumwabudu na kumsifu Mungu. Maandiko yamejaa maagizo na mahimizo mahususi kuhusu jinsi tunavyopaswa kuonyesha upendo na shukrani zetu kwa Mungu Mweza Yote kupitia sifa na shukrani zetu. 1. Zaidi ya aina zote za ibada, tunapaswa kumwabudu Mungu katika uhuru ambao Kristo ametupatia, Flp. 3:2-3. Tumewekwa huru katika Kristo dhidi ya kujaribu kumpendeza Mungu kwa uwezo wetu wenyewe, na sasa tunamwabudu kutoka moyoni, tukiwa tumejawa na shukrani na furaha. Je, tunapaswa kumwabuduje Mungu tunapokusanyika pamoja?

Made with FlippingBook - Share PDF online