Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
8 2 /
THEOLOJIA YA KANISA
ambayo yametokea, lakini kazi yetu haijatimizwa mpaka tuhubiri Injili “kwa kila kiumbe.” Hebu tuhakikishe kwamba Kanisa katika kizazi chetu halilegei katika kazi hiyo, bali tuongeze juhudi zetu maradufu ili kuhakikisha kwamba kila mtu anasikia Habari Njema na kuona nguvu za Mungu zikitenda kazi katikati yetu ili kuthibitisha ukweli wa ujumbe wetu. Baada ya kukiri na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (iliyopo kwenye viambatisho), omba maombi yafuatayo: Roho wa Mungu, tunakuomba uje juu yetu kwa nguvu na utufanye tushuhudie habari za Yesu hata miisho ya dunia. Tusaidie kuwapata waliopotea na kuwashawishi juu ya kweli ya Injili. Utusaidie kuwashuhudia walio karibu nasi, familia zetu na marafiki, lakini pia utusaidie kuwashuhudia wale walio mbali, walio tofauti na sisi kwa sababu ya mahali wanapoishi, lugha wanayozungumza, au utamaduni waliokulia. Utusaidie kuhubiri Injili kwa “kwa kila kiumbe” na tusichoke katika kazi hii tunapongojea kutokea kwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tunaomba haya kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
3
Weka kando daftari lako na nyenzo za kujifunzia, kusanya pamoja mawazo na tafakuri zako, kisha ufanye Jaribio la Somo la 2, Kanisa katika Ibada.
Jaribio
Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita: Waebrania 10:19-22.
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za Kukusanya
MIFANO YA REJEA
Je, Mungu Ana Upendeleo?
Katika mjadala wa historia ya Kanisa, mtu mmoja alitoa maoni katika darasa la ufuasi kwamba inaonekana kwamba Mungu ana upendeleo. Mataifa mengine yanaonekana kuwa tajiri na yenye ufanisi, huku mengine yakihangaika kila wakati kutafuta chakula, na yameteswa na hali mbaya ya hewa na vita. Baadhi
1
ukurasa 246 3
Made with FlippingBook - Share PDF online