Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 9 5
THEOLOJIA YA KANISA
Mungu ametuagiza kutangaza Habari Njema kwa wote, na kwamba kila mtu anayeamini atarithi uzima wa milele katika Yesu Kristo.
Hitimisho
» Yesu Kristo ni Mtumishi Mteule wa Mungu, ambaye kupitia kwake Mungu anawaokoa watu kutoka katika ulimwengu kwa ajili yake mwenyewe. » Mungu alichagua taifa moja liwe chombo ambacho kupitia hilo Masihi angekuja, taifa la Israeli, na jamii ya waaminio inayoundwa na Wayahudi na mataifa, Kanisa la Mungu katika Yesu Kristo. » Uteuzi wa Mungu unasisitiza utukufu wa ukuu wake, ajabu ya neema yake, asili muhimu ya uinjilisti, na uhakika wa wokovu wetu. Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yameibuka kutokana na maudhui ya video. Bila shaka, dhana ya uchaguzi wa Mungu ni ngumu na mtambuka, lakini yote yanakuwa wazi zaidi pale mtu anapotambua kwamba Mungu amemchagua Kristo kumwakilisha, na anatuchagua ndani yake. Hata hivyo, bado kuna maswali mengi muhimu kuhusu suala la Mungu kujua kabla ya yote, kusudi lake la kuchagua, na jinsi Mungu anavyofanya mambo yote pamoja kwa faida ya wale wanaomwamini, wale walioitwa kulingana na kusudi lake. Tafuta kuelewa dhana muhimu zinazohusishwa na mada hii, hasa ukisisitiza jukumu muhimu ambalo Kristo analo katika mjadala mzima wa uchaguzi wa Mungu. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, utumie Maandiko! 1. Ni katika maana gani Maandiko yanatufundisha kwamba Yesu Kristo ndiye Mtumishi Mteule wa Mungu, ambaye kupitia kwake Mungu anawaokoa watu kutoka katika ulimwengu kwa ajili yake mwenyewe? 2. Je, ni majina gani aliyopewa Yesu na mitume na manabii ambayo yanafunua uhusiano wa kipekee na usioweza kubatilishwa kati ya Yesu wa Nazareti na Yehova Mungu? 3. Je, tunapaswa kuelewaje uhusiano kati ya wale waliochaguliwa kwa ajili ya wokovu na Yesu Kristo? Ni kwa njia gani tunaweza kusema kwamba wateule wamechaguliwa kwa msingi wa muungano wao na Yesu, ambaye yeye mwenyewe ndiye Mtumishi Mteule wa kweli wa Mungu?
3
Sehemu ya 1
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 252 10
Made with FlippingBook - Share PDF online