Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 9 9
THEOLOJIA YA KANISA
2. Haturuhusiwi kubadilisha ujumbe; tunapaswa kutunza muktadha wa ujumbe bila kuubadilisha au kuuongeza (Gal. 1:8-9).
3. Kanisa linamshuhudia Yesu linapokwenda ulimwenguni, likiwa na uhuru wa kuweka ubunifu, likiwainjilisha waliopotea kwa kuhubiri Injili ya Kristo.
II. Kipengele cha pili cha Agizo Kuu ni ubatizo: Tunashuhudia kwa kubatiza. Kama washirika wa Kanisa tumeitwa kuwabatiza waamini wapya katika Kristo, yaani, kuwajumuisha na kuwaweka kama washirika katika Kanisa.
Tendo la kumkiri Kristo lazima lielekeze katika ushirika na watu wake. Ikiwa mtu anayedai kuwa Mkristo anakataa kujihusisha na watu wa Mungu, huenda ikawa ishara ya kwamba hajatubu na kuamini kweli kweli. Endapo hakuna dhamira ya dhati ya kujitoa kwa Kanisa, wokovu katika Kristo. Waamini wote wanaingizwa katika mwili wa Kristo kwa njia ya ubatizo. Tunapobatiza waamini wapya katika Bwana Yesu, tunawatambulisha kwa jumuiya yetu ya imani, hivyo ni lazima basi tuwaimarishe katika msingi, kweli za kwanza za imani, na kuwajumuisha kama kuna uwezekano kwamba hakuna
A. Kwanza, tumeamriwa kuwabatiza waamini wapya katika imani (Mk 16:15-16).
3
1. Mfumo wa kibiblia wa ubatizo:
a. Tunapaswa kubatiza katika jina la Mungu wa Utatu (Mt. 28:19).
b. Hii ni sawa na kubatizwa katika jina la Yesu Kristo. Ingawa wengine hudai kwamba hii ni tofauti na fomula ya utatu, maelezo ya Paulo katika Waefeso 4:5 kwamba “kuna ubatizo mmoja tu” yanadokeza kwamba ubatizo katika jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni sawa na kubatizwa “katika jina la Yesu Kristo,” au katika Yesu Kristo. Petro anawaambia Wayahudi siku ya Pentekoste katika Matendo 2:38, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
washirika muhimu katika kusanyiko la Kikristo.
Made with FlippingBook - Share PDF online