Theology of the Church, Swahili Student Workbook

1 1 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

zimegusa na kuathiri maisha yako. Je, umeweza kuhusisha kweli hii ndani ya maisha yako hadi sasa kwamba Mungu amekuchagua wewe katika Mwanawe – je, kweli hii inaathirije mawazo yako au kubadilisha jinsi unavyoomba au kuhusiana na waamini wengine, au watu wasioamini? Je, unahisi kujitoa kwa kina kwa Agizo Kuu? Mungu anakuita kuwa nini na kufanya nini ili utoe mchango wa juu uwezao katika kulitimiza, pale unapoishi na kuhudumu leo? Tumia muda fulani kumwomba Roho Mtakatifu azungumze nawe kuhusu kweli hizi na nyinginezo, na jinsi Mungu anavyoweza kukutaka uitikie kibinafsi. Maisha yako na huduma yako iko wazi na tayari kuguswa na mafundisho haya, ikiwa utakuwa makini kutafuta mahali ambapo kweli hizi zinaweza kuathiri moja kwa moja maisha yako. Tenga muda katika juma hili ili kwa ajili ya kutafakari kweli zilizomo katika somo hili, na umwombe Mungu ufahamu wa kuzitumia. Kuwa tayari kurejea wiki ijayo tayari kuwashirikisha wanafunzi wenzako yale utakayokuwa umejifunza kupitia muda wako wa kutafakari. Omba kwa Mungu Roho Mtakatifu akupe ufahamu wa upana na kina cha mafundisho ya mitume kuhusu asili ya fundisho la uchaguzi, na jinsi ukweli huu unavyoweza kuleta mapinduzi na kuathiri maisha yako. Pengine kuna baadhi ya mahitaji maalum ambayo Roho Mtakatifu ameyatokeza kupitia kujifunza kwako na mijadala ya somo hili. Uwe wazi kwa Bwana katika maombi; tafuta mtu wa kushirikiana naye katika maombi ambaye anaweza kushiriki mzigo wako na kuinua maombi yako kwa Mungu. Zaidi ya hayo, mwombe Mungu afanye upya maono yake kwa ajili yako katika mamlaka ya Agizo Kuu. Mwambie tena ili kwamba akuthibitishie wajibu wako katika kufanya wanafunzi – je, anakutaka uende, ufanye wanafunzi hapa, upande kanisa, uchunge, ushauri na kufundisha Wakristo wachanga, ubadili kazi, uhame makazi? Mtafute Bwana naye atakupa maelekezo maalum kuhusu kile anachotaka ufanye. Bila shaka, mwalimu wako yuko tayari sana kutembea nawe katika hili, na viongozi wako wa kanisa, hasa mchungaji wako, anaweza kuwa na ujuzi maalum wa kukusaidia kujibu maswali yoyote magumu yanayotokana na kutafakari kwako juu ya somo hili. Kuwa wazi kwa Mungu na umruhusu akuongoze jinsi apendavyo.

Ushauri na Maombi

3

Made with FlippingBook flipbook maker