Theology of the Church, Swahili Student Workbook

1 2 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

B. Kisha, Kanisa la Yesu Kristo ni takatifu. Kanisa limetakaswa, kufanywa takatifu, kupitia huduma ya Yesu Kristo.

1. Kanisa linafanywa takatifu, kutakaswa, na kutengwa kwa damu ya Yesu Kristo, Ebr. 10:10-14.

2. Kanisa linafanywa takatifu kupitia uwepo na huduma ya Roho.

a. 1 Kor. 3:16-17

b. Muunganiko huu na Mungu kwa njia ya Roho unafanywa kuwa msingi wa utii na usafi wa Kanisa, 1 Kor. 6:19-20.

3. Kanisa pia linafanywa takatifu, kutakaswa, na kutengwa kwa ajili ya milki ya Mungu na matumizi yake kupitia utii wake kwa mapenzi ya Mungu na Neno lake, Yoh. 17:15-19.

4

C. Tena, Kanisa ni “katoliki,” yaani la ulimwengu wote.

1. Kanisa lina tamaduni nyingi na ni la kihistoria: yaani, linajumuisha waamini kutoka katika tamaduni mbalimbali kutoka enzi na zama zote. Halizuiliwi na tamaduni, au lugha, au ukoo, au nchi.

a. Ufu. 5:8-10

b. Ufu. 7:9-10

Made with FlippingBook flipbook maker