Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 1 2 3
THEOLOJIA YA KANISA
2. Kanisa ni katoliki katika ujumuishi wake, linaundwa na wote wanaoweka imani yao katika Yesu Kristo, wawe Wayahudi au mataifa, wafungwa au watu huru, walio hai, waliokufa, au ambao bado hawajazaliwa.
a. Kol. 3:11
b. Gal. 3:28
D. Hatimaye, na pengine muhimu zaidi, Kanisa ni la kitume.
1. Imani na matendo ya Kanisa vinajengwa juu ya msingi wa kuchaguliwa kwa mitume na Yesu Kristo, (taz. Yoh. 17:6-9).
2. Kanisa limepewa mamlaka ya juu ya kuwa watetezi sahihi na wenye bidii wa mafundisho ya mitume, yaani mafundisho na mapokeo ya mitume.
4
a. 2 Thes. 3:6
b. Yuda 1:3
3. Pia, Kanisa la Yesu Kristo linafanya kazi kama wale wanaobeba chapa ya mamlaka ya kitume na kulinda kiini cha mamlaka hayo.
Kanisa la Yesu Kristo, kama Kanuni ya Imani ya Nikea inavyothibitisha, ni Kanisa moja, takatifu, katoliki, na la kitume.
a. Kama walinzi wa ushuhuda wa kitume, Kanisa linaitwa “nguzo na msingi wa kweli,” 1 Tim. 3:15-16.
b. Kanisa ni la kitume, yaani lililozaliwa kwa njia ya ushuhuda wao na watetezi wa mafundisho yao.
Made with FlippingBook flipbook maker