Theology of the Church, Swahili Student Workbook
1 2 4 /
THEOLOJIA YA KANISA
II. Sifa za Kanisa kulingana na mafundisho ya Matengenezo ya Kanisa: “Kanisa lipo mahali ambapo Neno linahubiriwa ipasavyo, sakramenti zinasimamiwa ipasavyo, na nidhamu imepangiliwa ipasavyo.” Wanatheolojia wa Matengenezo walikuwa wanakanisa katika karne ya kumi na saba ambao walitetea mafundisho ya msingi ya wokovu kwa neema kwa njia ya imani pekee na utoshelevu wa uwezo wa Yesu Kristo wa kuokoa. Pia waliandika kwa mapana juu ya asili ya Kanisa la kweli, ambapo waliifafanua kwa msingi wa mambo matatu: “Kanisa liko mahali ambapo Neno linahubiriwa ipasavyo, sakramenti zinatolewa kwa njia ipasayo, na nidhamu imepangiliwa ipasavyo.”
Mara Biblia inapotambuliwa kama Maandiko ya Kanisa, inakuwa mamlaka yake kuu iliyoandikwa, ndani ya Kanisa na sio juu au mbali nalo. Kila kitu katika Kanisa kinahukumiwa na Biblia. Hakuna chochote katika Kanisa kinachoweza kupingana nayo. Kila kitu katika Kanisa lazima kiwe cha kibiblia; kwa maana Kanisa, ili liwe Kanisa, lazima liwe aminifu kabisa na lenye kuakisi ukweli huo ambao Biblia yenyewe ni ushahidi wake wa kimaandishi. ~ Thomas Hopko, aliyenukuliwa katika Theodore G. Stylianopoulos. The New Testament: An Orthodox Perspective . Toleo la 1. Brookline, Massachusetts: Holy Cross Orthodox Press, 1997. uk. 55-56.
A. Sifa ya kwanza ya Kanisa la kweli kwa mujibu wa Wana-Matengenezo ni “Mahali ambapo Neno linahubiriwa ipasavyo.”
1. Sifa hii inahusiana na wazo la Matengenezo la sola Scriptura : Fundisho hili linasema kwamba hakuna magesterium , kanuni ya imani, au baraza linaloweza kuwa na mamlaka ya mwisho kwa habari ya imani na utendaji wa Kanisa zaidi ya Maandiko. Neno la Mungu ndilo kanuni yetu pekee isiyoweza kukosea ambayo ni msingi wa imani (kile tunachoamini) na utendaji (kile tulichoitiwa kufanya).
4
2. Wajibu wa waamini na viongozi wa Kanisa ni kulisha (na kujilisha) na kufundisha shauri kamili la Neno la Mungu. Katika mambo yote, Maandiko yanapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza katika maisha na utendaji wa Kanisa.
3. Kuthibitisha sola Scriptura (Maandiko pekee), bila shaka, haimaanishi kwamba hatupaswi kuchukua mapokeo ya Kanisa, au kwamba tunaweza kupuuza jukumu la Roho Mtakatifu katika kuelewa mafundisho ya Biblia. Sio suala la ama/au, bali suala la yote kwa pamoja.
Made with FlippingBook flipbook maker