Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 1 2 5

THEOLOJIA YA KANISA

B. Sifa ya pili ya Kanisa la kweli kulingana na mafundisho ya Matengenezo ya Kanisa ni “Mahali ambapo sakramenti zinatolewa ipasavyo.” Kanisa la kweli ni kusanyiko ambapo sakramenti (wakati fulani huitwa «maagizo» katika baadhi ya mapokeo) zinachukuliwa kama amri ya Yesu Kristo na kutekelezwa mara kwa mara kama sehemu ya maisha ya jumuiya ya Kikristo. Sakramenti mbili zinazotambulika ulimwenguni pote katika madhehebu ni ubatizo na Meza ya Bwana. Vigezo vya sakramenti kulingana na usomaji wa Maandiko wa Wana Matengenezo:

1. Kwanza, ilipaswa kuwa ilianzishwa (au kuamuriwa) na Yesu mwenyewe.

a. Kwa mfano, Yesu alijitiisha na kuanzisha ubatizo kama ishara ya wokovu. Katika Marko 16:15-16, Yesu anawaambia mitume wake waende ulimwenguni kote na kutangaza Injili kwa kila kiumbe. Alitamka kwamba wale watakaoamini na kubatizwa wataokolewa.

4

b. Yesu pia alizindua Meza ya Bwana kupitia sherehe yake ya Pasaka pamoja na wanafunzi wake kabla ya kifo chake, ona 1 Kor. 11:23-26.

2. Kisha, sakramenti za kweli zinapaswa kuonekana kama ishara ya imani inayookoa ya wale ambao wamejiunga na jumuiya ya agano ya Mungu.

a. Ubatizo ni kwa ajili ya wale ambao wametubu na kumwamini Yesu Kristo, wale ambao wamegeuka kutoka katika dhambi na kumgeukia Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.

b. Meza ya Bwana ilikusudiwa waamini, kama inavyoonekana wazi wazi katika mafundisho ya Paulo, ambapo anawahimiza Wakorintho kula mkate na kukinywea kikombe inavyostahili, yaani, katika ushirika kamili na Kristo, 1 Kor. 11.

Made with FlippingBook flipbook maker