Theology of the Church, Swahili Student Workbook

1 3 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

Kanisa katika Kazi Sehemu ya 2

Mch. Dkt. Don L. Davis

Asili ya kazi za Kanisa ulimwenguni inaweza kueleweka kwa kuchunguza picha mbalimbali za Kanisa zilizotajwa katika Agano Jipya. Kila moja ya taswira hizo inatupatia seti tofauti ya dhana za kutafakarisha juu ya jukumu na kazi ya Kanisa ulimwenguni. Tunaona uhusiano wa karibu wa Kanisa na Mungu kupitia picha za nyumba ya Mungu, mwili wa Kristo, na hekalu la Roho Mtakatifu. Tunalifahamu Kanisa kama wakala wa Ufalme wa Mungu kupitia picha ya Kanisa kama balozi wa Kristo. Hatimaye, tunaona Kanisa likifanya vita katika vita vya Mwana-Kondoo kama jeshi la Mungu vitani. Malengo yetu katika sehemu hii ya pili ya Kanisa katika Kazi ni: • Kuangazia kwa kina asili ya kazi za Kanisa ulimwenguni kwa kuchunguza picha mbalimbali za Kanisa zilizotajwa katika Agano Jipya. • Kuangalia kazi za Kanisa kupitia taswira ya nyumba ya Mungu, mwili wa Kristo, na hekalu la Roho Mtakatifu. • Kuchunguza kazi za Kanisa kupitia taswira ya ubalozi, Kanisa kama wakala wa Ufalme wa Mungu. • Kujifunza kuhusu Kanisa kupitia taswira ya jeshi la Mungu, kazi ya Kanisa kama kufanya vita katika vita vya Mwana-Kondoo. Picha hizi zinatoa ufahamu mkubwa wa jinsi tunavyopaswa kuelewa utambulisho wa Kanisa na kazi yake ulimwenguni leo. I. Kazi ya msingi ya Kanisa ni kutoa ushahidi wa kazi ya Mungu katika maisha ya kusanyiko lake: Kazi ya kwanza ya Kanisa ni kutangaza utukufu wa Mungu katika maisha na mahusiano yake. Kazi ya msingi ya Kanisa ni kuwa kitu, si kufanya kitu; Kanisa, kama watu wa Mungu, limeitwa kuonyesha ubora wa maisha unaoakisi utukufu wa Yeye aliyeliumba hapo kwanza. Agano Jipya linatupatia taswira nyingi za Kanisa, ambazo zote zinatupatia ufahamu wa asili ya kazi ambazo tunapaswa kufanya ili kumtukuza Mungu kama watu wake.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

4

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

Made with FlippingBook flipbook maker