Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 1 3 3

THEOLOJIA YA KANISA

A. Kwanza, kama nyumba ya Mungu, tunapaswa kuishi kama kaka na dada kwa umoja kama familia pendwa ya Mungu mwenyewe.

Kulingana na Paulo katika Tito 2:14, Yesu alijitoa mwenyewe dhabihu kwa ajili ya watu wake, Kanisa ili “atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.” Ndiyo, tunapaswa kuwa na bidii kwa ajili ya matendo mema ambayo, kulingana na Waefeso 2:10, tuliumbwa kuyafanya. Na Petro anaweka wazi katika 1 Petro 2 kwamba nia na msukumo mkuu nyuma ya kazi hizi ni kuakisi ubora na tabia ya Mungu. Sisi ni mali yake, na tunaishi ili kutangaza ubora wa tabia yake duniani. “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu” (1 Pet. 2:9).

1. Maandiko yanatangaza kwamba sisi ni watoto wa Mungu, wanafamilia wa nyumba na familia ya Mungu, Efe. 4:1-3.

2. Tunapaswa pia kufanya kazi zinazoleta ushirikiano na umoja katika kushuhudia habari njema ya Injili ya Yesu Kristo, Flp. 1:27-28.

B. Kisha, kama mwili wa Kristo ulimwenguni, tunapaswa kuakisi maisha ya Yesu katika mahusiano yetu sisi kwa sisi na kati yetu na majirani zetu.

1. Ni haki na wajibu wa kila Mkristo na kila kanisa la mahali pamoja kuwakilisha na kutoa mchango katika kazi ya Yesu ulimwenguni, Rum. 12:4-6a.

4

2. Paulo anathibitisha kwamba kuna mwili mmoja, imani moja, na tumaini moja la wito wetu. Hivyo basi, kwa kuzingatia umoja huu, tunapaswa kutubu kwa ajili ya kila mwelekeo wa ubinafsi wa kufikiria mila zetu au shughuli zetu ni muhimu zaidi kwa Mungu kuliko za wengine. Ni tendo lisilo la uadilifu kupuuza au kubeza michango ya waamini wengine, na lazima tutafute kujipatanisha nao ili kutimiza makusudi ya Mungu ulimwenguni, Efe. 4:1-6.

C. Hatimaye, kama hekalu la Roho Mtakatifu, tunapaswa kufuata matendo ya utakatifu na utii kama mahali patakatifu ambapo jina la Mungu linajulikana na kutukuzwa.

1. Katika matendo yetu yote pamoja kama waamini, tunapaswa kufanya kazi na kuishi maisha ambayo yanadhihirisha usafi wa Mungu na utii wetu, Ebr. 12:14.

Made with FlippingBook flipbook maker