Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 1 4 7

THEOLOJIA YA KANISA

Kihistoria, vyanzo vitatu muhimu vimesaidia hasa katika Kanisa kuleta maana ya asili na utendaji wake wa kweli katika ulimwengu. Kwanza, vigezo vya Kanisa kulingana na Kanuni ya Imani ya Nikea vinasisitiza kuhusu Kanisa kuwa moja, takatifu, la kitume na la ulimwengu wote. Ufafanuzi wa Kanisa kulingana na mafundisho ya Matengenezo ya Kanisa unasisitiza kuhubiriwa kwa Neno, uzingatiaji wa sakramenti na utaratibu sahihi wa nidhamu. Kuhusiana na ukweli wa mafundisho, kanuni ya Mtakatifu Vincent inasisitiza mambo ambayo yameaminiwa kila mahali, siku zote, na wote. Asili ya Kanisa na kazi zake pia zinaweza kueleweka kwa kuchunguza picha au mifano mbalimbali ya Kanisa iliyotajwa katika Agano Jipya. Tunaona uhusiano wa karibu wa Kanisa na Mungu kupitia taswira ya nyumba ya Mungu, mwili wa Kristo, na hekalu la Roho Mtakatifu. Tunalifahamu Kanisa kama wakala wa Ufalme wa Mungu kupitia taswira ya Kanisa kama balozi wa Kristo. Hatimaye, tunaona Kanisa likifanya vita katika vita vya Mwana-Kondoo kama jeshi la Mungu katika vita. Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo yanayohusiana na mada zilizoletwa katika somo hili la Kanisa katika Kazi , unaweza kujaribu vitabu hivi: Bonhoeffer, Dietrich. Life Together. San Francisco: Harper Collins Publishers, 1954. Ellis, Carl F., Jr. Beyond Liberation. Downers Grove: InterVarsity Press, 1983. Ortiz, Juan Carlos. Disciple: A Handbook for New Believers. Orlando: Creation House Publishers, 1995. Perkins, John. Let Justice Roll Down. Ventura, CA: Regal Books, 1976. Sider, Ronald J. Cry Justice: The Bible Speaks on Hunger and Poverty. Downers Grove: InterVarsity Press, 1980. Utawajibika sasa kutumia maarifa ya moduli hii katika mazoezi ya vitendo ambayo wewe na Mkufunzi wako mtakubaliana. Matokeo ya moduli hii ya Kanisa ni mengi na makubwa: fikiria njia zote ambazo mafundisho haya yanaweza kuathiri maisha yako ya ibada, maombi yako, mwitikio na utendaji wako katika kanisa lako, mtazamo wako kazini, na maeneo mengine mengi. Unachopaswa kufahamu sasa, unapoanza kuhusianisha kweli hizi na maisha na huduma yako mwenyewe, ni maeneo yanayo husiana moja kwa moja na yale ambayo hayahusiani moja kwa moja na maisha na huduma yako. Kweli hizi kuhusu asili na kazi ya Kanisa zinatumika moja kwa moja katika maisha yako kama mfuasi unayekua na kukomaa katika kanisa lako; Mungu anataka kukutumia kama mtu unayesaidia wengine kuelewa

Marejeo ya Tasnifu ya Somo

Nyenzo na Bibliografia

4

Kuhusianisha Somo na Huduma

Made with FlippingBook flipbook maker