Theology of the Church, Swahili Student Workbook
1 4 8 /
THEOLOJIA YA KANISA
asili ya maisha ya kweli ya Kanisa, hata katika kusanyiko lako. Kadiri unavyoziona kweli hizi vizuri zaidi, ndivyo utakavyoweza kuzieleza vizuri zaidi kwa wengine, na kuzidhihirisha katika mtindo wako wa maisha na huduma kwa waamini wengine katika kusanyiko lako la Kikristo. Kama ilivyo katika kila kipengele cha ukuaji na huduma, itakuwa muhimu sana kwamba utafute kuunganisha mafundisho haya na maisha na kazi yako yote. Huu ndio umuhimu wa kazi yako ya huduma kwa vitendo. Iliundwa kimakusudi kwa kuzingatia mambo haya, na katika siku zinazofuata utakuwa na fursa ya kuwashirikisha watu wengine maarifa haya katika maisha halisi na hali halisi za huduma. Omba kwamba Mungu akupe utambuzi wa njia zake unapowashirikisha wengine maarifa yako kupitia kazi yako. Kama mshirika wa mwili wa Kristo, na kama kiongozi katika Kanisa, lazima umwombe Bwana kwa habari ya ufahamu wake, hekima, na uwezo wa kutumia kweli hizi maishani mwako, na kwa wale ambao Mungu anataka uwahudumie. Je, kuna masuala yoyote, watu, hali, au fursa zinazohitaji kuombewa kama matokeo ya kujifunza kwako somo hili? Je, ni masuala gani hasa au watu ambao Mungu ameweka katika moyo wako ambao wanahitaji dua na maombi mahususi kulingana na maarifa ya somo hili? Chukua muda wa kutafakari hili, na upokee usaidizi unaohitajika kwa njia ya ushauri na maombi kwa ajili ya yale ambayo Roho amekuonyesha. Omba hasa kuhusu jinsi vigezo na taswira za Kanisa zinavyoweza kuwa halisi katika maisha yako mwenyewe, maisha ya jumuiya ya Kikristo, na jinsi ambavyo Mungu angetaka kukusaidia kuzungumza na wengine kweli hizi kuhusu watu wake.
Ushauri na Maombi
4
MAZOEZI
Hakuna kazi ya kukabidhi.
Kukariri Maandiko
Hakuna kazi ya kukabidhi.
Kazi ya Usomaji
Kufikia wakati huu, unapaswa kuwa umeshughulikia maelezo yote na Mshauri wako kuhusu maamuzi yako kwa habari ya kazi yako ya huduma kwa vitendo na ile ya ufafanuzi wa Maandiko. Unapaswa kuwa umeainisha, kufanyia maamuzi, na kuhakikisha mapendekezo yako yamepitiwa na kukubaliwa na mkufunzi wako. Ikiwa kwa sababu yoyote haujawasiliana na mkufunzi wako na kumpatia maelezo mahususi ya mapendekezo yako kuhusu kazi zako, fanya hivyo haraka
Kazi Zingine
Made with FlippingBook flipbook maker