Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 1 4 9

THEOLOJIA YA KANISA

iwezekanavyo. Hakikisha kwamba unapanga mapema namna ya kutekeleza kazi zako, ili kuepuka kuchelewesha kazi hizo.

Mtihani wa mwisho utakuwa wa kwenda nao nyumbani, na utajumuisha maswali yaliyochukuliwa kutoka katika majaribio matatu ya kwanza, maswali mapya kutokana na maarifa yaliyofundishwa katika somo hili, na maswali ya insha ambayo yatahitaji majibu yako mafupi kwa maswali muhimu yenye lengo la kuhusianisha somo na huduma na maisha. Pia, wakati wa mtihani unapaswa kujiandaa kuandika au kutamka aya zilizokaririwa katika kozi hii. Ukimaliza mtihani wako, tafadhali mjulishe mkufunzi wako na uhakikishe kuwa anapata nakala yako. Tafadhali zingatia: Ufaulu wako katika moduli hii hauwezi kupimwa na kujulikana kama hautafanya mtihani wa mwisho na kukusanya kazi zote na kuzikabidhi kwa mkufunzi wako (Fomu ya Ripoti ya Usomaji, kazi za kihuduma, kazi za ufafanuzi wa Maandiko, na mtihani wa mwisho). Bwana Yesu amekuwa akikusanya kutoka duniani kote watu ambao siku moja watakuwa bibi-arusi wake mwenyewe, jamii mpya ya wanadamu, maridadi iliyounganishwa na Mungu kwa imani ndani yake, ili wapate kuishi katika utukufu kama watumishi wake katika mbingu mpya na nchi mpya. Ingawa mikusanyiko yetu midogo ya kiinjili, masomo ya Biblia, vikundi seli, mikusanyiko ya ibada, na mikutano mingine inaweza isionekane kuwa aina ya mikutano inayoakisi sifa ya jamii mpya ya wanadamu walioitwa na Mungu, ukweli wa mambo ni kwamba sisi ni wa Mungu. Tutaishi milele katika mji mpya, uliojengwa kwa mikono ya Bwana, ambapo Mungu atatukuzwa milele, katikati ya dunia ambayo itarejeshwa kwenye utukufu na fahari yake ya kwanza ya Edeni. Sisi ni sehemu ya familia ya milele ya Mungu, na kazi yetu ni kumwakilisha Kristo na Ufalme wake kwa hadhi, ubora, na uwazi wote anaostahili. Bwana Mungu atumie kweli za moduli hii kusaidia kuwatayarisha watu wanaoakisi upendo na neema ambayo amemimina juu yetu kupitia Mwanawe Yesu Kristo. “Loo! Watakatifu watakapokuja wakiingia...”

Taarifa Kuhusu Mtihani wa Mwisho

Neno la Mwisho kuhusu Moduli hii

4

Made with FlippingBook flipbook maker