Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 1 8 1
THEOLOJIA YA KANISA
KIAMBATISHO CHA 16 Theolojia ya Kanisa Don L. Davis na Terry Cornett ©1996 World Impact Press
Kanisa Ni Jamii Ya Kitume Ambamo Neno Linahubiriwa Ipasavyo
I. Jamii ya Wito
A. Maana muhimu ya Kanisa ni Ekklesia : wale ambao “ wameitwa kutoka ” katika ulimwengu ili “ kuitwa kuingia ” katika Jamii Mpya. 1. Kama Wathesalonike, Kanisa limeitwa kutoka katika ibada ya sanamu ili kumtumikia Mungu aliye hai na limeitwa kumngoja Mwanawe kutoka mbinguni. 2. Kanisa limeitwa ili liwe la Kristo (Rum. 1:6). Yesu anazungumza kuhusu Kanisa kama “ ekklesia yangu” yaani “walioitwa” ambao ni mali yake ya pekee (Mt. 16:18; Gal. 5:24; Yak. 2:7). 3. Vipengele vya wito wa Mungu: a. Msingi ni nia ya Mungu ya kuokoa (Yoh. 3:16, 1 Tim. 2:4). b. Ujumbe ni Habari Njema ya Ufalme (Mt. 24:14). c. Wapokeaji ni “yeyote atakaye” (Yoh. 3:15). d. Njia ni kupitia imani katika damu iliyomwagwa ya Kristo na kukiri ubwana wake (Rum. 3:25; 10:9-10; Efe. 2:8). e. Matokeo yake ni kuzaliwa upya na kuwekwa ndani ya mwili wa Kristo (2 Kor. 5:17; Rum. 12:4-5; Efe. 3:6; 5:30).
B. Kanisa limeitwa kutoka .
1. Limeitwa kutoka ulimwenguni: a. Ulimwengu uko chini ya utawala wa Shetani na unasimama kinyume na Mungu.
Made with FlippingBook flipbook maker