Theology of the Church, Swahili Student Workbook

1 8 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

b. Kuokoka na kuingizwa katika Kanisa la Kristo kunahusisha toba ( metanoia ) na uhamisho wa kiapo cha utii na uaminifu kutoka ufalme wa giza kuelekea ufalme wa nuru. c. Kanisa lipo kama wageni na wapitaji ambao wako “ndani ya” lakini sio “wa” mfumo huu wa ulimwengu. 2. Kuitwa kutoka katika dhambi: a. Wale walio ndani ya Kanisa wanatakaswa, wametengwa kwa ajili ya matendo matakatifu, ili waweze kuuishi wito wao kama watakatifu wa Mungu (1Kor. 1:2; 2 Tim. 1:9, 1 Pet. 1:15). b. Kanisa lazima liwe tayari kwa ajili ya kusudi la Mungu na kutumiwa na Yeye (Rum. 8:28-29; Efe. 1:11; Rum. 6:13). c. Kanisa lazima lilete utukufu kwa Mungu pekee (Isa. 42:8; Yoh. 13:31-32; 17:1; Rum. 15:6; 1 Pet. 2:12). d. Kanisa lazima liwe na sifa ya utii kwa Mungu (2 The.1:8; Ebr. 5:8 9; 1 Yoh. 2:3). 1. Wokovu na maisha mapya a. Msamaha na utakaso wa dhambi (Efe. 1:7; 5:26; 1 Yoh. 1:9). b. Kuhesabiwa haki (Rum. 3:24; 8:30; Tito 3:7) ambapo Mungu anatutangaza kuwa hatuna hatia kwa habari ya adhabu ya sheria yake ya kiungu. c. Kuzaliwa upya (Yoh. 3:5-8; Kol. 3:9-10) ambapo “utu mpya” unazaliwa ndani yetu kwa njia ya Roho. d. Utakaso (Yoh. 17:19; 1Kor. 1:2) ambao ndani yake “tunatengwa” na Mungu kwa ajili ya utakatifu wa maisha. e. Utukufu na Uzima wa Milele (Rum. 8:30, 1 Tim. 6:12; 2 The.2:14) ambapo kwa huo tunabadilishwa kuwa kama Kristo na kutayarishwa kuishi milele mbele za Mungu (Rum. 8:23; 1Kor. 15:51-53; 1 Yohana 3:2).

C. Kanisa limeitwa kwenye :

Made with FlippingBook flipbook maker