Theology of the Church, Swahili Student Workbook

1 9 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

b. Kuongozwa na Roho ili ibada yake ielekezwe kwa Mungu pekee (2 Kor. 3:6; Gal. 5:25; Flp. 3:3). c. Kuonyesha sifa ya Mungu ya kutobadilika katika namna ambazo zinafaa kwa tamaduni na haiba za waabudu fulani (Matendo 15). 6. Kanisa linaabudu kwa utaratibu ufaao, likihakikisha kwamba kila tendo la ibada linajenga Mwili, na kusimama sawasawa na Neno la Mungu ( 1Kor. 14:12, 33, 40; Gal. 5:13-15, 22-25; Efe. 4:29; Flp. 4:8). D. Ibada ya Kanisa inaleta uzima na ustawi: 1. Afya na baraka vinakuwa sehemu ya jamii ya ibada (Kut. 23:25; Zab. 147:1-3). 2. Jamii ya ibada inachukua tabia ya Yule anayeabudiwa (Kut. 29:37; Zab. 27:4; Yer. 2:5; 10:8; Mt. 6:21; Kol. 3:1-4; 1 Yoh. 3:2). A. Kanisa ni kusanyiko la wale wanaoshiriki katika Agano Jipya. Agano Jipya hili: 1. Lina Yesu Kristo kama Mpatanishi, Kuhani Mkuu, na limepatikana na kutiwa muhuri kwa damu yake (Mt. 26:28; 1 ​Tim. 2:5; Ebr. 8:6; 4:14-16). 2. Namna pekee ya kulianzisha na kulishiriki ni kwa njia ya kuchaguliwa na Mungu kwa neema yake (Rum. 8:29-30; 2 Tim. 1:9; Tito 1:1; 1 Pet. 1:1). 3. Ni agano la amani ( Shalom ) ambalo linatoa njia ya kumkaribia Mungu (Eze. 34:23-31; Rum. 5:1-2; Efe. 2:17-18; Ebr. 7:2-3). 4. Linaadhimishwa kwa uzoefu wa kipekee katika Meza ya Bwana na Ubatizo (Mk. 14:22-25; 1 Kor. 10:16; Kol. 2:12; 1 Pet. 3:21).

V. Jamii ya Agano

Made with FlippingBook flipbook maker