Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 1 9 1

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

5. Kwa imani, huwahesabia haki na kuwapa washiriki wa Agano lake haki ili sheria za Mungu ziwekwe mioyoni mwao na kuandikwa katika nia zao (Yer. 31:33; Rum. 1:17; 2 Kor. 5:21; Gal. 3:21-22; Flp. 1:11 ; 3:9; Ebr. 10:15-17; 12:10-11; 1 Pet. 2:24).

B. Agano hili hutuwezesha kuuelewa na kuupokea utakaso wa Kikristo: 1. Haki: mahusiano sahihi na Mungu na wengine (Kut. 20:1-17; Mika 6:8; Mk. 12:29-31; Yakobo 2:8). 2. Kweli: imani sahihi kuhusu Mungu na wengine (Zab. 86:11; Isa. 45:19; Yoh. 8:31-32, 17:17; 1 Pet. 1:22). 3. Utakatifu: matendo mema kwa Mungu na kwa wengine (Law. 11:45; 20:8; Mhu. 12:13; Mt. 7:12; 2 Kor. 7:1; Kol. 3:12; 2 Pet. 3:11). C. Kusudi la Agano Jipya ni kuliwezesha Kanisa kuwa kama Kristo Yesu: 1. Yesu ndiye kielelezo kipya kwa wanadamu: a. Adamu wa pili (Rum. 5:12-17; 1 Kor. 15:45-49). b. Ambaye Kanisa limeumbwa kwa mfano wake (Rum. 8:29; 1 Yoh. 3:2). c. Maisha yake, tabia yake, na mafundisho yake ndicho kipimo cha imani na utendaji (Yoh. 13:17; 20:21; 2 Yoh. 6, 9, 1 Kor. 11:1). 2. Agano hili limewezekana kwa dhabihu ya Kristo mwenyewe (Mt. 26:27-29; Ebr. 8-10). 3. Huduma ya kitume ya Agano Jipya inakusudiwa kuwafanya waamini wafanane na Kristo (2 Kor. 3; Efe. 4:12-13).

Made with FlippingBook flipbook maker