Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 1 9 5

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

1. Shauku ya Mungu ya kupatanisha inathibitishwa kwa kuwatuma manabii wake na katika siku za mwisho, kwa kumtuma Mwanawe (Ebr. 1:1-2). 2. Kufanyika mwili kwa Yesu, maisha, kifo, na ufufuo wake ni matendo ya mwisho ya upatanisho kutoka kwa Mungu kumwelekea wanadamu (Rum. 5:8). 3. Injili sasa ni ujumbe wa upatanisho, unaowezekana sasa kupitia kifo cha Kristo, ambao Mungu hutoa kwa wanadamu (2 Kor. 5:16-20). B. Kanisa ni jamii ya watu binafsi na makundi ya watu ambao wanapatanishwa wao kwa wao kwa utambulisho wao wa pamoja kama mwili mmoja. 1. Kwa kifo chake Kristo aliwaunganisha watu wake waliozaliwa kwa uzao mmoja (1 Yoh. 3:9), waliopatanishwa kama raia pamoja na washiriki wa jamii mpya ya wanadamu (Efe. 2:11-22). 2. Jamii ya Kanisa inawatendea washirika wote wa nyumba ya Mungu kwa upendo na haki licha ya tofauti za rangi, matabaka, jinsia, na tamaduni kwa sababu wameunganishwa kihalisia kwa kushiriki kwao katika mwili wa Kristo (Gal. 3:26-29; Kol. 3:11). C. Kanisa ni jumuiya inayojishughulisha na upatanisho miongoni mwa watu wote. 1. Kanisa hufanya kazi ya balozi anayewaalika watu wote kupatanishwa na Mungu (2 Kor. 5:19-20). Kazi hii ya utume inaweka msingi wa shughuli zote za upatanisho za Kanisa. 2. Kanisa linadumisha upatanisho na watu wote. a. Kwa sababu Kanisa limeamriwa kuwapenda adui zake (Mt. 5:44 48). b. Kwa sababu Kanisa ni jamii inayofanyika Mwili ambayo inatafuta, kama Kristo, kujitambulisha pamoja na wale waliojitenga nalo.

Made with FlippingBook flipbook maker