Theology of the Church, Swahili Student Workbook

1 9 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

c. Kwa sababu Kanisa linaakisi Ufalme wa Mungu na kufanya kazi kwa ajili ya maono ya Ufalme huo ambamo watu, mataifa, na uumbaji wenyewe watapatanishwa kabisa na kuwa na amani (Isa. 11:1-9; Mika 4:2-4; Mt. 4:17; Mdo. 28:31). d. Kwa sababu Kanisa linatambua mpango wa milele wa Mungu wa kuvipatanisha vitu vyote mbinguni na duniani chini ya kichwa kimoja, Bwana Yesu Kristo, ili kwamba Ufalme huo ukabidhiwe kwa Mungu Baba ambaye atakuwa yote katika yote (Efe. 1:10) ; Rum. 11:36; 1Kor. 15:27-28; Ufu. 11:15, 21:1-17). D. Kanisa ni jamii ya urafiki: urafiki ni sehemu muhimu ya upatanisho na maendeleo ya kiroho. 1. Ukomavu wa kiroho huleta urafiki na Mungu (Kut. 33:11; Yakobo 2:23). 2. Ufuasi wa kiroho huleta urafiki na Kristo (Yohana 15:13-15). 3. Umoja wa kiroho unadhihirishwa katika urafiki na watakatifu (Rum. 16:5, 9, 12; 2 Kor. 7:1; Flp. 2:12; Kol. 4:14; 1 Pet. 2:11; 1 Yoh. 2:7; 3 Yoh. 1:14). A. Jamii ya Kanisa inateseka kwa sababu ipo ulimwenguni kama “kondoo kati ya mbwa-mwitu” (Luka 10:3). 1. Kuchukiwa na wale wanaomkataa Kristo (Yohana 15:18-20). 2. Kuteswa na mfumo wa ulimwengu (Mt. 5:10; 2 Kor. 4:9; 2 Tim. 3:12). 3. Kipekee ni jamii ya maskini, wenye njaa, wanaolia, wanaochukiwa, waliotengwa, wanaotukanwa, na waliokataliwa (Mt. 5:20-22). 4. Imejengwa juu ya kielelezo na uzoefu wa Kristo na mitume (Isa. 53:3; Lk. 9:22; Lk. 24:46; Mdo 5:41; 2 Tim. 1:8; 1 The.2:2).

VIII. Jamii ya Mateso

Made with FlippingBook flipbook maker