Theology of the Church, Swahili Student Workbook

2 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

Hitimisho

» Kanisa lilifunuliwa katika kusudi kuu la Mungu: azma yake ya kujiletea utukufu kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe kupitia jamii mpya ya wanadamu kwa njia ya agano lake na Abrahamu. » Kanisa lilifunuliwa awali katika kufunuliwa kwa siri kuu ya kujumuishwa kwa mataifa katika Kristo Yesu. » Kanisa lilifunuliwa awali katika picha ya Mungu ya watu wake, laos wa Mungu. Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengineyo ambayo yametokana na video. Kuanzia hapa, lazima tuwe wazi kabisa kuhusu mapenzi ya Mungu ya kuleta utukufu na heshima kwa nafsi yake, na jinsi jambo hilo linavyohusiana na kusudi lake kuu la kuwakomboa watu kutoka duniani kote kwa ajili yake. Mungu anatoa ishara ya wazi kuhusu kusudi lake la milele kupitia agano lake na Ibrahimu, ufunuo wa siri kuhusu ushiriki wa mataifa katika Habari Njema, na uumbaji wa watu wake, picha ya jamii mpya ya wanadamu itakayokuja. Kuwa wazi na ufupishe majibu yako, kadri inavyowezekana tumia Maandiko kuunga mkono hoja zako! 1. Ni kwa njia gani Mungu alifanya agano na Ibrahimu ili kwamba, kupitia kwake, familia zote za dunia zipate kubarikiwa? 2. Maandiko yanashuhudia nini kuhusu kusudi kuu la Mungu juu ya uumbaji wake, ufunuo wake mwenyewe, na ukombozi wake kwa wengine kwa ajili yake? Kwa nini Mungu aliumba ulimwengu? 3. Ni aina gani ya siri inayozungumziwa katika Warumi 16, Waefeso 3, na Wakolosai 1 kuhusu kusudi la Mungu la ukombozi? 4. Nini kinachoonyeshwa na Mungu kuhusu kusudi lake kwa mataifa linapokuja suala la kusudi lake la kuvuta watu kutoka duniani kote kwa ajili yake? Ni jinsi gani kusudi hili linaonyeshwa katika agano ambalo Mungu alifanya na Abrahamu? 5. Ni kwa njia gani Israeli ni chombo na njia ya Mungu kumleta Masihi duniani? Jinsi gani Israeli inaonyesha kupitia uhusiano wake na Mungu picha ya wazi ya watu wa Mungu, Kanisa?

1

Sehemu ya 1

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook flipbook maker