Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 3 7
THEOLOJIA YA KANISA
³ Kanisa lilitabiriwa katika ufunuo wa siri kuu ya ujumuishwaji wa mataifa katika Kristo Yesu. Kupitia mitume na manabii, Mungu amefanya ijulikane kwa kizazi hiki na kwa falme na mamlaka nia yake ya kuwaokoa mataifa kwa imani kupitia Mwanawe, na kuwajumuisha katika familia yake milele. ³ Kanisa lilitabiriwa katika picha ya Mungu ya watu wake, laos wa Mungu. Kupitia watu wa Israeli, Mungu ametupa ishara ya jamii mpya ijayo, inayojumuisha mataifa na Wayahudi. ³ Ingawa Mungu ametoa nafasi maalum kwa Kanisa kama watu wake, hajawaacha Israeli wala kufuta wito na uteule wao. Pindi Mungu atakapokamilisha wokovu wa mataifa, ataokoa masalia ya Israeli, kama inavyoelezwa katika Warumi 9-11. ³ Wokovu, soteria , unamaanisha kuokolewa, kukombolewa, au kufanywa kuwa salama. ³ Dhambi hututenga na Mungu na kutufanya kupotea, yaani, “kukatiliwa” nje ya upendo na ulinzi wa Mungu, na kweli yake. ³ Matokeo ya kuwa “wapotevu” mbali na Mungu ni: mauti ya kimwili na ya kiroho, utumwa wa dhambi, na hukumu/adhabu. ³ Kuunganishwa na Kristo (kupitia imani katika maisha yake, kifo chake, na ufufuo wake) ndiyo njia ambayo Mungu huturudisha katika uhusiano naye. ³ Kuunganishwa na Kristo kunatatua matatizo matatu yaliyosababishwa na dhambi. Kifo cha Kristo kinalipa deni la kisheria tulilokuwa tunadaiwa kwa kuvunja sheria ya Mungu, kwa kuwa Kristo alibeba adhabu yetu msalabani. Ushindi wa Kristo dhidi ya Shetani unatufungua kutoka katika utumwa wa dhambi. Na ushindi wa Kristo juu ya mauti unatuhakikishia uzima wa milele kwa sababu tumeunganishwa na maisha yake. ³ Kwa kuunganishwa na Kristo, mtu hujiunga na watu wote wa Mungu ambao watapata uzima katika Ufalme mpya. Utambulisho wa Mkristo unategemea ukweli kwamba sasa yeye ni sehemu ya Kanisa, ambalo ni watu walioteuliwa na Mungu.
1
Sasa ni wakati wa kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu dhana ya somo hili, Ufunuo kivuli wa Kanisa katika historia na Maandiko. Ili kupata kwa kina utajiri wa dhana ya Kanisa, ni muhimu kuelewa kwamba nia ya Mungu ya kujitwalia watu duniani kote kwa ajili ya Jina lake ni nia ya kale na yenye shauku
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi
Made with FlippingBook flipbook maker