Theology of the Church, Swahili Student Workbook
3 8 /
THEOLOJIA YA KANISA
kubwa. Lengo la sehemu hii kwenu kama wanafunzi ni ili mpate kushughulika na mpango mkuu wa Mungu kwa ulimwengu. Ni maswali gani maalum uliyonayo kutokana na mafundisho uliyopokea? Pengine baadhi ya maswali yafuatayo yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako binafsi, mahususi na muhimu zaidi. * Kwa nini ni muhimu kwa kiongozi wa kanisa kuelewa na kuwa na uwezo wa kueleza kuhusu ufunuo wa awali wa Kanisa katika kusudi kuu la Mungu la kujitukuza ndani ya watu wake? Kuna uhusiano gani kati ya kusanyiko lako la mahali na shauku ya Mungu ya kuinua watu wapya watakaokaa naye milele? * Kuna matokeo gani ya kivitendo ya dhana kwamba Mungu alikusudia hata mataifa kujumuishwa katika kusudi lake la ukombozi kwa ulimwengu? Hili linasema nini kuhusu nia ya Mungu kwa makanisa ya mahali kuwa wazi, huru dhidi ya ubaguzi, upendeleo, na dhana potovu za kikabila? * Ikiwa wote wanaomwamini Kristo ni sehemu ya watu wake, tunapaswa kuwaonaje hata wale waamini wanaokusanyika katika makanisa madogo sana, hata yale yaliyo katika vibanda vidogo mijini ambapo Yesu anaheshimiwa na kuabudiwa? Makanisa madogo mijini yanawezaje kudai kuwa sehemu ya ( laos ) watu ambao Mungu aliahidi kuinua kama watu wake maalum? * Kwa nini inaonekana kwamba baadhi ya makundi ya watu wa Mungu yana uzito na hadhi kubwa zaidi kuliko mengine? Mwelekeo huu ulioenea kati ya vikundi vya Kikristo unadhoofishaje wazo kwamba Mungu anafanya kazi ya kujitwalia watu kutoka mataifa yote ya dunia kwa ajili yake mwenyewe? * Kwa nini inaweza kuwa muhimu kwa kiongozi wa kanisa kuelewa kwamba Mungu amekuwa akifanya kazi ya kuwakusanya watu wake kwa karne nyingi? Ni uongo gani ambao adui anaweza kumwambia kiongozi aliyekata tamaa au aliyekosa matumaini kwamba jitihada zake za kujenga kanisa haziwezi kufanikiwa? * Kwa nini inaweza kuwa muhimu kwa mhudumu wa mijini kuelewa shauku ya Mungu ya kufanya Kanisa kuwa mahali pa kila mtu, hata kwa watu wa mataifa, yaani, wale wanaohusishwa katika Biblia na uasherati, ibada ya sanamu, na dhambi? Hii inaweza kumaanisha nini kwa wale waliotengwa na jamii leo? * Kwa nini inaweza kuwa muhimu kwa mkristo mtendakazi mwaminifu kuthibitisha kusudi la Mungu la kujikusanyia watu kwa ajili yake? Je, hiyo inamaanisha kwamba tunapaswa kupunguza bidii yetu ya kufanya wengine kuwa wanafunzi wa Kristo?
1
Made with FlippingBook flipbook maker